FAIDA YA KILIMO CHA MAPAPAI KIUCHUMI

                                   FAIDA YA KILIMO CHA MAPAPAI KIUCHUMI

PAPAI

Hili ni aina ya zao la matunda linalopatikana katika familia ya caricaceae na linajulikana kwa jina la kisayansi carica papaya

Papai ni moja ya matunda ambayo huchukua muda mfupi hadi kufikia mavuno. Huchukua muda wa miezi 6-7 kufikia mavuno.

Matunda katika mpapai utokeza katika kila jani na mpapai kwa wiki moja unauwezo wa kutengeneza majani mawili na kwa makadilio mpapai huanza kutengeneza maua katika jani la 32 hii ikimaanisha ni baada ya wiki nne.

FAIDA KIUCHUMI

Ekari moja inauwezo wa kuwa na mipapai 1000-1200. Mavuno ya mapapai kwa miezi 6 – 7 kwa mavuno ya kwanza ni tani 40 – 60 ikiwa kila mpapai unaweka matunda 40 hadi 50 kwa miezi 6 – 7. Baada ya mavuno ya kwanza, mavuno ya mapapai hayana msimu hivyo yataendelea ndani ya miaka mitano katika uangalizi mzuri wa mipapai yako hadi kufikia kipindi ambacho mpapai wako utapokufa..

JINSI YA KUJUA FAIDA

Kwa matunda 40 – miti 1000 jumla ya matunda 40,000 yatavunwa

Bei ya papai Tsh. 500 kwa papai

500 x 40,000 = 20,000,000/=

Hivyo kwa kila mwezi ni tsh. 2,500,000/= kwa mipapai ya miezi 6 kufikia mavuno.

Mahitaji

Mahitaji ya mipapai kwa mwezi hayazidi 500,000/-= hivyo unauhakika wa kupata faida ya 2,000,000/= kwa mwezi kutokana na zao la mapapai.

FURSA YA SOKO LA PAPAI

Inapofika swala la soko mambo huwa tofauti kwani watu wengi kabla ya kuanza kulima tunauliza kuna soko?  Swali lengine utasikia kuna soko la uwakika.?

Kupitia nakala hii ya kilimo cha papai utagundua jinsi ya kutatua changamoto za soko hususani kilimo hiki cha papai.

Nitakufundisha njia tatu muhimu za kutatua changamoto za soko ambazo ni;

Njia ya kwanza.

Kama umeamua kulima papai ni vema kuangalia mambo makuu mawili la kwanza  ni kulima tofauti na msimu ili kusiwe na mlundikano wa matunda na njia ya pili soma number mbili hapo chini.

Njia ya pili.

Hakikisha unatoa zao bora kwani unapokuwa na matunda bora kuna uwezekano wa kupunguza madalali na pia unaweza kuvutia wateja wengi kufuata matunda shambani.

Njia ya tatu.

Tafuta njia mbadala ya kusambaza mazao yako.kama umeamua kufanya kilimo biashara basi unahitaji kutafuta njia mbadala ya kusambaza mazao yako mwenyewe unahitaji kuwa na mazao bora ambayo yatawafanya watu wayafurahie.

Note; hizo ndoo njia tatu muhimu za kutatua changamoto za soko .

Sasa tujifunze soko lako ni lipi?

Kutokana na faida na uitaji wa matunda jamii ya mapapai kwenye mwili wa binadamu,tunda hili limekuwa likitajika kwa wingi sana sehemu mbali mbali.Soko lake linaweza kuwa:

Masokoni

Kumekuwa na uhitaji mkubwa sana wa papai sokoni kumbe unaweza kuhuza papai zako sokoni

Mashuleni

Hapa tunaongelea kwenye vyuo mbali mbali kuna mahitaji makubwa sana ya zao hii kwani watu awajui ni mahara gani wanaweza kupata kumbe kuna uwezekano mkubwa wa kuhuza papai maeneo ya vyuoni.

Mahoteli na Migahawa

Hapo ndoo usiseme mahitaji ya matunda ya papai ni makubwa kuliko tunavyofikiria.

Mahospitalini.

Kuna hospitali nyingi wanahitaji tunda hii kwani sio tunda ni dawa pia kwa hiyo mahitaji ya tunda hii katika maeneo ya hospitali ni makubwa sana. Kwa watu wanaojishughulisha na huduma za vyakula kwenye sherehe na matukio mbalimbali.

Ili kujua uhalisia wa biashara hii kwa soko la ndani ni vyema basi kuangalia mzunguko wa biashara ya papai kuanzia shambani mpaka linapouzwa

Maeneo mengine; kwenye tasisi, wizara mbalimbali, maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu.

Ufafanuzi wa kina

Katika ekari moja unaweza panda miche ya mapapai kuanzia 1000(elfu moja) mpaka 1200,

Mche mmoja wa papai unauwezo wa kutoa mapapai wastani wa matunda 86 mapaka 100 kimakadirio,

Bei ya papai sokoni ni wastani wa shilingi za kitanzania 1000 mpaka 4000,bei hii inategemeana na ukubwa na uwepo wa mapapai sokoni,

Bei ya papai kwa jumla shambani ni wastani wa shilingi za kitanzania 500 mpaka 1000

.Wakulima wengi na wataalamu wanasema kwamba papai kwenye ekari moja unaweza pata 1000.Ili kwendana na uhalisia tuta piga hesabu kwa wastani wa miche ya mipapai 300 kwa hekari.Na mavuno ya matunda ya papai kwa mche iwe 50.Vigezo hivi tumechukua wastani wa chini ili kuweza kumhamasisha mpenda fursa ya zao hili.

Wastani wa ekari=1,

Miche ya mapapai kadirio la chini =300,

Matunda ya mapapai kwa mche =50,

Bei la papai moja sokoni kadirio la chini ni =800,

Bei la papai kwa jumla shambani kadirio la chini ni=400,

Mavuno ya msimu mmoja kwa bei ya sokoni=300*50*1000=15,000,000/=

Mavuno ya msimu mmoja kwa bei ya shambani=300*50*500=7,500,00/=

Hesabu hizi ni kadirio la chini kabisa.Endapo utalima kwa kufata taratibu zote na ukiongozwa na wataalamu wa kilimo cha mapapi basi itakuwezesha kupata mazao mengi yaliyo kwenye ubora unaotakiwa.

CHAKUZINGATIA

Ili kufanya kilimo hichi kibiashara yapo mambo mengi ambayo  ni vyema ukitaka kuingia kwenye fursa hii uwe umeshavizingatia,vitu hivyo ni:

Eneo la ardhi (unaweza nunua,au kukodisha),

Uhakika wa udongo unaowezesha kilimo hichi (Ni vyema ukapima udongo wako kabla hujaanza kilimo chako)

Upatikanaji wa maji (Kwa shughuli za kilimo),

Mbegu,( uwe na mbegu bora)

Nguvu kaz i(Mtu wa kuwa anasimamia mradi wako )

Mtaalamu wa kilimo(Kwa ajili ya kuwa anakupa mwongozo na ushauri wa mambo yote ya kuzingatia katika kilimo cha mapapai) n.k

CHANGAMOTO

Zipo changamoto kadha wa kadha kwenye kilimo hichi cha mapapi.Changamoto hizo ni:

Matunda kuoza au kuharibika haraka

Kutokuwa na njia bora za kuhifadhi matunda yasiaribike haraka,

Ndege,wanyama na wadudu mbali mbali wanaoweza kuharibu matunda haya,

Ukosefu au uchache wa viwanda vya kusindika juisi ya papai,

Ukosefu wa mbinu za masoko kwa wakulima wa zao hili n.k

SULUHISHO

Matunda kuoza au kuharibika haraka inabidi mfanya biashara wa zao hili kuwa na vyombo vya kuifadhi mazao yasiaribike haraka,pia mwuzaji anaweza kuamua kushusha bei kidogo pindi mtunda haya yanapokuwa yamekaa muda mrefu ili kupunguza hasara zinazoweza jitokeza.

Pia ni wachache waojua kwamba mapapai pia nichakula kizuri cha mifugo mbali mbali kama kuku,bata,bata mzinga na nguruwe hivyo mfanya biashara hii anaweza boresha ili kuona namna gani ya kupunguza hasara hii isijitokeze.

Kupambana na ndege na maadui wengine wa mapapai,ni vyema kuangalia namna ya kujengea labda wavu au kuwa na net inayoweza wazuia ndege na maadui wengine wa zao hili.Zipo namna nyingi za kupambana na maadui hawa ni vyema mkulima akaangalia njia iliyo na gharama nafuu kwa kuangalia ukubwa wa mradi alio nao.

Tunda hili linatumiwa na asilimia kubwa ya watanzania nazani ni vyema mkulima kutembelea sehemu zenye fursa ya kuuza matunda haya na kuangalia namna gani anaweza ingia nao mkataba ili kuweza kupata soko bora.

Viwanda vya kusindika juisi ya mapapai ni changamoto na suluhisho lake ni watu kuwekeza kwenye fursa hii ya usindikaji wa mapapai ili kuweza patia jamii huduma hii.

Zipo njia nyingi sana za kutatua matatizo haya fursatz.com tunaimanin kwamba sehemu yoyote yenye changamoto ndiko sehemu yenye fursa ya biashara nyingine.Ni jambo jema kuangalia changamoto kama sehemu ya kuanzisha fursa kama njia ya suluhisho ya changamoto hiyo.

GHARAMA ZA UWEKEZAJI

Kununua au kukodi ardhi (gharama za kukodi zinaanzia 70,000-100,000) ikitegemeana na eneo lilipo,kununua inategemea gharama za eneo husika,

Kulima shamba na kuandaa mashimo kwa hekari ni mambo nanayoweza kugharimu fedha isiyozidi 300,000/=,

Miche ya mapapai gharama zake kwa kununua mche mmoja ni shilingi 3000,

Kununua papai na kuziandaa mbegu mwenyewe itakuondolea gharama za kunua miche ,

Gharama za kumlipa mwangalizi wa shamba ambayo hii inawezafanyika kwa maelewano,hapa pia unaweza weka pia gharama za uendeshaji na utunzaji wa mradi husika.

Gharama za upimaji wa udongo.

Zipo gharama nyingi lakini hizi zitakuwa zimekupa mwanga kwaajili ya kuitazama fursa hii kwa mapana zaidi.Tunaimani endapo uwekezaji wa kina utafanyika basi unaweza kukidhi soko la ndani na nje pia.Ni jukumu la kila mpenda fursa kuitambua fursa hii na kuifanyia utafiti wa kina ili kuona jinsi gani inavyoweza kumfaidisha

MAHITAJI

Hali ya hewa inayofaa kwa mipapai ni ya kitropik ambayo haina baridi kali na joto kiasi . Udongo usiotuamisha maji maji yakisimama kwa masaa 48 tu mpapai unaweza kufa, wenye rutuba ya kutosha kwa sababu mipapai haina mzizi mkuu haihiyaji udongo wenye kina kirefu, kipindi cha jua kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8

bila kumwagiliwa maji kama hakuna mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii huongeza ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema sokoni

Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mwingi kwani huvunjika kirahisi, kama unashamba la mipapai itakubidi kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea, vibiriti ( leucaena Spp ) na miembe pia inafaa. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai

Kuendelea kupanda mipapai kwenye shamba moja kunaweza kusababisha usugu wa magonjwa, nashauri baada ya miaka 3 hadi 5 ubadilishe zao hili angalau kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa

Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya michungwa, pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta , alizeti na mboga mboga yanaweza kulimwa

Kwa kaida kwenye mipapai kuna mipapai dume, majike na yenye jinsia zote

(multiplesex/hermaphrodite) ambayo huwa na mapapai marefu zaidi, na pia kuna isiyoeleweka ambayo huwa na mapapai mafupi sana

MBEGU

Kusanya mbegu toka kwenye mapai makubwa na yaliyo komaa na kuiva, kausha mbegu vizuri kbla ya kupanda, kama utapata mbegu za kununua ni vizuri zaidi, baada ya kukausha hakikisha unazipanda ndani ya wiki moja

KUOTESHA MBEGU

Kuna wanaopendelea kuotesha mbegu kwanza na kisha kuhamishia miche shambani, sehemu ya kuoteshea iandaliwe miezi miwili kabla, mbegu zioteshwe kwenye kina kati ya sentimeta 1 au 2 chini ya udongo wenye rutuba au pakiti za plastiki, kiwango bora cha joto ni sentigredi 21 au 27 na itachukua kati ya wiki 1 hadi 4 kwa mbegu kuota, kwenye kila pakiti weka mbegu 2 ahdi 3. Panda mbegu zako kwenye kitalu kwa umbali wa sentimeta 3 toka shimo hadi shimo na sentimeta 15 kati ya mistari, hakikisha maji hayatuami kabisa, pia unaweza kupiga dawa ya copper oxychloride gramu moja katika lita moja ya maji ilikukinga miche yako na fangasi

UOTESHAJI WA MOJA KWA MOJA

Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea ya kuku sehemu ya kupandia, mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia kukinga mipapai na magonjwa. Panda mbegu 3 hadi 5 kila shimo maana miche mingine inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume

KUHAMISHA MICHE TOKA KWENYE KITALU

Miche ihamishiwe shambani ikiwa na urefu wa sentimeta 20 hadi 40, kama udongo unatuamisha maji panda kwenye matuta yenye urefu wa sentimeta 40 hadi  60 mashimo yawe na ukubwa wa sentimeta 45 upana na sentimeta 30 kina na shimo lichanganywe na udongo na samadi bila kuacha kisahani cha maji, umbali ni mita 3 kwa 3 kwani mipapai inahitaji jua la kutosha

KUPUNGUZA MIPAPAI

Baada ya miezi 3 hadi 5 baada ya kupanda mipapai itatoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana na mingine itabidi ipunguzwe na hasa midume, mipapai yenye jinsi zote inatakiwa isizidi asilimia 10hadi 20 na midume ibaki mmoja katika kila mijike 25, mimea yenye magonjwa pia inabidi ingolewe.

RUTUBA YA UDONGO

Weka kiasi chakilo 2 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa mwaka ili kuongeza ukuaji na uzazi, mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama matandazo na h ii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee.

Faida ya kutumia mbolea ya samadi

Samadi husaidia kuongeza rutuba ardhini vilevile  itaubadili udongo uwe katika hali nzuri zaidi kwa kustawisha mimea.

Manufaa mengine ya mbolea ya samadi ni kuwa inaufanya udongo kuwa katika hali ya nzuri ya kuweza kuyashikilia maji au unyevu kwa muda mrefu.

Minyoo waishio udongoni ambao husababisha kuwepo nafasi kwa ajili ya hewa kupenya kwa urahisi na vijidudu vya bakteria ambavyo huozesha mbolea na kubadili hewa kuwa katika hali ya chumvichumvi zinazotumiwa na mimea hupata mazingira mazuri kwa maisha yao katika udongo uliotiwa samadi.

Note; wataalamu wanasema kuwa ubora wa samadi inategemea jinsi ilivyokuwa imetunzwa zizini au kibandani kwani chumvi nyingi hasa zile za nitrates kuwa zinapotea kwa urahisi kwa maji ya mvua, kutokana na kitendo chake cha kuyeyuka mara tu zinapolowa maji.

MAGUGU

Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia uoataji wa magugu, magugu yangolewe yakiwa machanga na epuka kuchimbua chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu, njia nzuri ni kuweka matandazo kwenye shamba lote ili kuzuia outaji wa magugu

UANGALIZI

Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ingolewe na kuchomwa au kufukiwa chini ikiwa itabainika kuwa na maonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya fangasi na virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji nakipato chako

Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.

Ondoa mapapi yote ambayo ya takuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha yale yenye afya tu

Weka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na hasa wakati wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjike

Mipapai ikitunzwa inaweza kuishi mika mingi, ila kwa ajili ya mazao bora ondoa mipapai na upande mingine baada ya kila miaka mitatu (3) kwani mpapai unapo kuwa mkubwa basi rutuba yote huishia kwenye mti wenyewe

Mengineyo unaweza kutumia mbolea za maji kama;

D.i grow green kwa ajili ya kupandia baada ya siku 14 hadi 21 baada ya kupanda.

Mkojo wa sungura kwa ajili ya wadudu na kurutubisha udongo.

Sababu ya mpapai kuwa dhaifu na kuangusha maua.

Hii husababishwa na

 1. Hali ya hewa.  Joto likiwa juu sana hupelekea sana maua kuanguka na pale ambapo joto hushuka chini sana pia hupelekea kuanguka.
 2. Wadudu na magonjwa. Maua huanguka  kwa kupata usumbufu wa wadudu na magonjwa.
 3. Kutomwagilia maji ya kutosha.
 4. Ukosefu wa nitrojeni. Mmea hutaji nitrojeni kwa ajili ya kutengeneza maua na majani kuwa yenye afya kwa ajili ya kuimarisha mmea kwa mmea kukosa kiasi cha kutosha cha naitrojeni pale ambapo maua yatajitengeneza yataishia kuanguka kwani yatakuwa dhaifu.
 5. Mche kutoa maua mengi. Hutokea mara kwa mara mche kutoa maua mengi sana  kwa wakati wa kutengeneza maua na pia hutokea pale uwekaji wa mbolea za naitrojeni unapokuwa mkubwa.
 6. Mmea kukosa mwanga wa kutosha. Vitu ambavyo uchangia sana ukuaji mzuri na hatimaye mmea kuweka maua katika mche ni pamoja na mwanga wa kutosha ambao husaidia sana kwa maua kutoa mbali na hapo mkulima hataendelea kuona tatizo au changamoto hii katika kilimo cha papai.

Namna ya kukabiliana na changamoto hii.

 • Fanya umwagiliaji wa kuzingatia ukuaji wa mmea.
 • Hakikisha udongo wako unakuwa na kiasi cha kutosha cha rutuba
 • Zuia mashambulizi yote yatokanayo na wadudu na magonjwa kwa kutumia njia mbili za kuzuia wadudu na magonjwa ikiwemo zile za madawa na za kibailojia.
 • Panda mmea wako katika mahala ambapo kuna mwanga wa kutosha.

Zingatia mambo aya muhimu hili uweze kufanikisha au kufanikiwa katika kilimo cha papai.

 • Njia ya kwanza kukuza mmea.
 • Njia ya pili ni wakati gani wa kupanda.
 • Njia ya tatu ni mahali pa kukuza.
 • Njia ya nne upandaji na ukuzaji.
 • Njia ya tano ni wateja.

Sababu ya mpapai kuanguka au kudondoka yakiwa machanga.

Miti kudondosha matunda ni jambo la kawaida endapo itapandwa katika ardhi isiyokuwa na virutubisho sahihi.

Kwa kifupi.

Ardhi ikiwa na kiwango kidogo cha magneziamu (Mg) pia ikiwa na kiwango cha juu cha Potasiam (P) na Boron (B).  hivyo kabla hujandaa shamba kwa ajili ya kilimo cha papai ni muhimu kupata ushauri wa kitaalamu wa aina ya udongo ili upate uhakika wa kujua unachotaka kukipanda.

Kuna wakati miti ya papai hudondosha matunda wakati yakiwa bado machanga kitendo ambacho ni hasara kwa mkulima.

Baadhi ya miti hiyo huanza kudondosha matunda muda mfupi baada ya kuanza kuzaa na hii hutokea baada ya maua kujitenga na tunda.

Hii imekuwa changamoto kubwa kwa wakulima na wengi wamekuwa wakiulizia kuhusu kadhia hii.

Ili kuweka sawa jambo hili tutaongelea papai kupukutisha maua na matunda kabla hayakomaa.

 • Hali ya hewa au mvua kuzidi
 • Magonjwa ya mmea
 • Wadudu
 • Uhaba wa rutuba na mbolea na pia uwekaji mbolea ya kukuzia katika kipindi kisichotakiwa.

MUHIMU

Zingatia sana katika uchaguzi wa mbolea, chagua mbolea ambayo ina kiwango kikubwa cha P na K ukichagua mbolea ilio na kiwango kikubwa cha N hii inaweza kuharibu maua.

Unaweza pia kutumia mbolea ya mabaki ya mimea na wanyama katika kukuza miti yako.

Aidha uongezaji mbolea kiholela pia unaweza kuathiri mmea

Ni muhimu kuzingatia sababu zinazosababisha mti kudondosha matunda kabla hayajakomaa kwani matunda yanapondoka huchochea mti kuzalisha kemikali ya ethylene ambayo husababisha matunda mengine kuendelea kudondoka.

IMEANDALIWA NA ALLY SAID KIHORO

EMAIL. Kihoro48@gmail.com

Whatsap no.+255678970256

Leave a Reply