FAIDIKA NA KILIMO CHA BIASHARA CHA MPUNGA KUPITIA MFUMO WA KILIMO SHADIDI CHA MPUNGA.

HISTORIA YA MFUMO WA KILIMO SHADIDI CHA MPUNGA

Wakulima wengi wa mpunga kipindi cha nyuma walikuwa wakipata wastani wa gunia tano adi saba za mpunga kwa Ekari moja kutokana na kilimo cha asili cha mpunga .Lakini baada ya kupata elimu kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uholanzi (SNV) kwa kushirikiana na washirika wake, wakulima  hao sasa ekari ile ile wanavuna gunia kati ya 15 hadi 20 wanapolima kilimo shadidi cha mapunga.

Mpunga ambao ukikobolewa tunapata mchele ni moja ya chakula kikuu cha Watanzania ukichukua nafasi kubwa ya nyuma ya mahindi. Hata hivyo, matumizi ya mchele kama chakula yamekuwa yakiongezeka licha ya uzalishaji wake kuendelea kuwa wa kiwango cha chini. Kwa mantiki hiyo, kilimo shadidi ni muhimu kikatekelezwa na wakulima nchini kote kutokana na umuhimu wake.

Taarifa zilizopo zinaonesha kwamba kilimo shadidi cha mpunga kilivumbuliwa kwa mara ya kwanza nchini Madagascar na Padri Henri de Laulanié miaka takriban 20 iliyopita. Tangu hapo, kanuni za kilimo hicho zimeonesha uwezo mkubwa kila mahala duniani zilipotumika na kuleta mageuzi makubwa ya kilimo cha mpunga. Wastani wa mavuno kwa dunia kama mkulima atatumia vizuri kanuni za kilimo shadidi, pamoja na mbegu bora kabisa ni tani nne (magunia 40 kwa Ekari).

KILICHOJIFICHA NYUMA YA KILIMO SHADIDI.

 1. Mkulima kupunguza msongamano wa miche kwani anatakiwa kupanda mche mmoja mmoja kwa nafasi ili mizizi na shina vipate nafasi ya kutosha kukua.
 2. Katika kilimo hiki kuna matumizi ya maji kidogo kwa kilimo cha umwagiliaji, hivyo mkulima anaweza kutumia maji ya ziada kwa shughuli nyingine.
 3. Mkulima anaweza kupanda eneo kubwa kwa kutumia mbegu chache.
 4. Mazao yatatoka mengi na ni vigumu kupata magonjwa (mara mbili zaidi ya njia ya kawaida). Njia hii inaboresha ardhi na palizi lake linaifanya ardhi iwe na rutuba zaidi.

 

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA.

Kiwango kidogo cha mbegu kinatumika katika kilimo hiki (kilo 2 hadi 3 kwa ekari).  Eneo la mita 40 za mraba kwa ekari moja ya bustani ya miche linatosha.  Mche mmoja kwa kila tuta hutumika  Katika mita moja ya mraba yanatakiwa matuta 16.  Mahitaji makubwa ya upaliliaji kama mtu atalima kiasili huwa yamepunguzwa. Ukuaji wa mimea na mizizi unaboreshwa kupitia njia ya upaliliaji.

Maji ya kuelea shambani kwa muda mrefu hayahitajiki.  Asilimia 40 hadi 50 ya maji ya kumwagilia yanahifadhiwa. Kunakuwa na matumizi kidogo ya nguvu za umeme wakati wa umwagiliaji endapo maji yanahitajika na kuna miundombinu inayotumia umeme.

Mimea hustahimili kutoanguka au kulala chini kwa sababu ya upepo mkali au kibunga.  Kunakuwa na mazao mengi ya nafaka na mabua, yaani mabaki ya mimea.Panda miche michanga kwa uangalifu katika mazingira ya udongo ulio na hewa ya kutosha.Miche isizame katika udongo uliolowa maji. Kwa kuwa idadi ya miche itakuwa michache katika mfumo huu wa ukuzaji mpunga, unaweza kutumia bustani iliyoinuliwa kwa ukuzaji wa miche.

 • Kiwango cha mbegu kinachopendekezwa kama ilivyoelezwa hapo juu ni kilo 3 kwa ekari moja.
 • Mita 40 za mraba za bustani iliyoinuliwa inatosha kwa upandaji katika ekari moja.
 • Tengeneza bustani ya kuinuka kima cha sentimita 5 kwa kila 1m x 5m, yaani bustani 8 zinahitajika kwa sehemu ya 40m2 (mita 40 za mraba).
 • Matumizi ya mbolea asili (samadi) ya shambani iliyoiva vizuri yafanywe kwa uangalifu.
 • Usitumie mbolea ya ziada baadaye katika bustani iliyoinuliwa kwa udongo ulio na rutuba ya kutosha. Kama sivyo, weka mbolea ya dukani ya ‘DAP’ kiasi cha gramu 760 kwa kila ekari (gramu 95 kwa kila bustani ya 5m2 iliyo muinuko pamoja na udongo.
 • Tandaza magunia yaliyokuwa ya mbolea ya dukani (polythene bags) juu ya bustani kwa ulainifu.
 • Jaza udongo ukilainisha juu ya magunia hayo kwa kima cha mpaka sentimita 4 kwa urefu.
 • Mbegu zihifadhiwe na dawa ya ‘Pseudomonas’ kwa kiwango cha gramu 10 kwa kila kilo ya mbegu.
 • Tumia gramu 200 za mbolea asili ya ‘Azophos’ kwa kila kilo 3 za mbegu.
 • Changanya ‘Pseudomonas’ na mbolea asili ya ‘Azophos’ na mbegu za mpunga kwa kutumia mchanganyiko wa mpunga huo na maji kwa saa 24.
 • Weka mbegu hizo kwa saa 24 katika magunia ya mkonge kwa minajili ya uchipuzaji. • Panda gramu 375 za mbegu iliyooteshwa katika kila mita 5 za mraba za bustani iliyoinuka.
 • Mwagilia maji kwa kutumia kopo. Maji ambayo husimama kando kando ya bustani iliyoinuka yaweza kutumika.
 • Funika bustani kwa kutumia mali ghafi inayopatikana kirahisi popote ulipo kama vile vifuu vya nazi, mabua ya mpunga na uiondoe siku tatu baada ya kupanda mbegu iliyooteshwa. Usimamizi wa miche
 • Ng’oa miche pamoja na udongo wake kutoka kwenye bustani ili miche iweze kunawiri kwa haraka.
 • Usumbufu kidogo wa mizizi wakati wa kung’oa utasaidia sana miche kukua kwa haraka.
 • Panga miche katika kisanduku cha mbao na ukisafirishe hadi shambani utakapopandia, ili unapopanda iwe rahisi kutawanisha miche. Kumbuka, bustani ya miche inaweza kutayarishiwa mbali na shamba.

Inaweza kuwa karibu na nyumba ya mkulima kwa ajili ya ulinzi na usimamizi. Wakati wa kuhamishia miche shambani, ipangwe kwenye vijisanduku vidogo ili kurahisisha usafirishaji. Ni sharti miche isipitishe zaidi muda wa dakika thelathini (nusu saa) kabla ya kupandwa. Mbinu hii ya kukuza miche na kuisafirisha husaidia kuokoa wakati, kati ya bustani na shambani. Shamba linavyotakiwa

 • Sawazisha shamba utakapopanda machipukizi yako vizuri. Yaani ni muhimu liwe tambarare.
 • Mbegu zenye nguvu zikipandwa katika shamba lisilosawazishwa na kuwa tambarare kuna uwezekano mkubwa wa kuoza.
 • Tengeneza mitaro midogo kwa ajili ya kurahisisha mkondo wa maji.
 • Acha hatua ya sentimita 25 za mraba (25cm x 25cm) kutoka tuta la mmea hadi mwingine kwa upanz i (upandaji). Upandaji wa kimraba
 • Ni sharti mche mmoja peke yake upandwe kwa kila tuta.
 • Usipande katika shimo la kimo cha ndani sana.
 • Upandaji mraba wa sentimita 25 x 25 huhakikisha nafasi ya kutosha
 • Katika upandaji huu kifaa cha kutia alama kinachozunguka (rolling marker) au kamba iliyowekwa alama vinaweza kutumiwa kwa upandaji ili kupata vipimo hatua sahihi. Kupanda mche mmoja kwa kila tuta ina faida kubwa sana kwa mmea. Mimea huwa na afya zaidi kwa ajili ya ushindani mdogo kati ya mimea na mmea katika matumizi wa hewa, mwangaza na virutubishi vya udongo.

Hivyo basi kila mmea una uwezo mkubwa mno wa kuzalisha au kuchipuza mikombo (tillers). Kupanda miche kwa mraba husaidia kuwa na nafasi tosha ya kupitishia chombo cha kupalilia mimea kiitwacho kwa kimombo rotary weeder au paddy weeder machine. Upaliliaji unaotumia mashine

 • Utumiaji wa mashine ya kupalilia ni mojawapo ya hatua muhimu sana katika mfumo huu maalum. Mashine za kupalilia zinatumika kila baada ya muda wa siku kumi tangu siku ya kupandikiza miche (jumla ya mara nne kwa uhai wa mpunga shambani).
 • Vibarua watatu wanatosha kupalilia ekari moja kwa mara moja (kwa siku moja).
 • Magugu hung’olewa na mashine na kuoza na hivyo kuwa mbolea.
 • Mara kwa mara, udoango husumbuliwa, jambo ambalo lina manufaa kwa mmea. Kimsingi palizi ni muhimu na hivyo mkulima anatakiwa kuhakikisha anaifanya ili kupata mazao mengi na pia kuifanya kwa vifaa maalumu. Kwa hatua hii magugu hung’olewa na kuzikwa kwenye mchanga ili iwe kama mbolea (green manure). Pili, kila wakati kifaa hiki kinapotumika, udongo husumbiliwa na kugeuzwa, huku hewa zaidi ikipenya kwenye mchanga.

Hewa hii hufaidisha sana mizizi na vijiumbe vilivyo kwenye udongo. Kazi ya tatu ya kifaa hiki cha kupalilia ni ya kukatakata mizizi ya mimea iliyo kando kando. Kitendo hiki huhakikisha mizizi mipya inakua na yenye uwezo mkubwa wa kujitafutia chakula na madini muhimu toka kwenye mchanga. Kazi hizi tatu muhimu za chombo cha kupalilia ni kusababisha mimea kuchipuza mikombo zaidi na pia shina huwa na nguvu ya kuhimili upepo na kimbunga Umwagiliaji

 • Hakikisha hakuna maji ya kusimama katika shamba na pia udongo udhibitiwe kwa kuwa katika hali ya unyevu au ukavu.
 • Mwagilia maji mpaka kina cha sm 2.5 baada ya mistari ya mipasuko kutokea kwenye udongo. Inaweza kuchukua siku saba baada ya kumwagilia maji hadi udongo upasuke. Ikiwa hivyo basi kumwagilia maji kwenye shamba lako itakuwa ni kila baada ya siku saba hadi mpunga uanze kuzaa ambapo utamwagilia shamba mara tu kidimbwi cha maji shambani kinaponyauka.
 • Badilisha zamu za kulowesha na ukaushaji ili hewa ipenye kwenye udongo na kuongeza ukuaji wa mizizi na kuendeleza utendaji kazi wa vijiumbe vya aradhini (micro-organisms).

FAIDA ZA KILIMO SHADIDI.

 1. Gharama ya kulimia ni ya chini sana,
 2. Kiwango kidogo cha mbegu kutumika (kilo 2 hadi 3 kwa ekari),
 3. Eneo la mita 40 mraba kwa ekari moja ya bustani ya miche linatosha,
 4. Mche mmoja kwa kila tuta hutumika,
 5. Matuta kumi na sita (16) peke yake kwa mita moja mraba,
 6. Mahitaji ya ufanyikazi kwa upaliliaji hupunguzwa,
 7. Ukuwaji wa mimea na mizizi utaboreshwa kupitia njia ya upaliliaji,
 8. Maji ya Kuelea kwa shamba kwa muda murefu hayatahitajika,
 9. Asilimia 40 hadi 50 ya maji ya kumwagilia yanahifadhiwa,
 10. Matumizi kidogo ya nguvu za umeme wakati wa umwagiliaji maji iwapo

unahitajika,

 1. Kiwango cha juu cha ukuaji wa mizizi,
 2. Idadi kubwa zaidi ya mizizi mieupe inayotumia maji kidogo,
 3. Matumizi ya madini ya udongoni ni bora zaidi,
 4. Kiwango cha juu cha uchipuzi wa mikombo na vichwa vya nafaka,
 5. Mazao mengi yanayotokana na na idadi kubwa ya mikombo (tillers),

vichwa vya nafaka (productive tillers) na nafaka yenyewe,

 1. Mimea kustahimili kuanguka au kulala chini kwa sababu ya upepo mkali

au kibunga,

 1. Mazao mengi ya nafaka na mabua (mabaki ya mimea), na
 2. Faida ya kiwango cha juu.

 

 

 

 

 

Leave a Reply