Hizi Hapa Faida Za Asali Za Nyuki Wadogo Kwa Undani Zaidi Soma Hapa Ili Ujue.

Na Jesca Pelembela,Morogoro
Idara ya Biologia ya Misitu SUA, imewashauri wananchi kutumia asali bora iliyotengenezwa na nyuki wadogo kwa sababu ni asali iliyo na virutubisho vingi na muhimu kwa matumizi, pia hutumika kama dawa ya magonjwa mbali mbali.
Akizungumza na mwangukuonline mtaalamu wa mambo ya nyuki na uvunaji wa asali, Bwana Michael Singila, amesema kuwa asali ya nyuki wadogo ni nzuri zaidi kwa sababu nyuki wadogo hutengeneza asali yenye virutubisho vingi ukilinganisha na asali ya nyuki wakubwa.
“kuna utofauti kati  ya asali ya nyuki wadogo na nyuki wakubwa, asali ya nyuki wadogo ni nyepesi, ina rangi ya kahawia na ina radha ya chachu na uchungu kidogo, tamu na ina limao pamoja na ukakasi, asali ya nyuki wakubwa inakuwa rangi nyeusi, nyeupe, njano pamoja na rangi ya dhahabu” Amesema Bwana Singila.
Bwana Singila amesisitiza kuwa asali ya nyuki wadogo ni nzuri kwa matumizi, lakini  asali bora ni ile iyokomaa na kurinwa shambani kwa kukamuliwa na si ile ambayo hurinwa na kupikwa, kwa sababu asali ikipikwa hupoteza virutubisho.
Amesema ili kutambua kuwa asali ni bora na haijachemshwa ni lazima uonje na kunusa, endapo asali imechemshwa utahisi harufu ya moshi na kama haijachemshwa utahisi radha ya maua, na asali hiyo itakuwa bora kwa kuwa virutubisho vilivyomo ndani ya asali vitakuwa havijaharibiwa.

Leave a Reply