JE NAWEZAJE KUJUA IDADI YA SAMAKI WAKUWEKA KWENYE BWAWA LANGU

Suleimani Pandauyag:

Ni muhimu sana kwa mfugaji samaki kuweza kujua idadi sahihi ya vifaranga ambavyo anaweza kuweka kwenye bwawa lake kwaajili ya kupata matokeo mazuri kabisa kwenye bwawa lake (optimization of the pond productivity). Japokuwa kumekuwa na nadhari mbalimbali zinazoelezea idadi ya vifaranga vya kuweza kuwekwa kwenye bwawa (stocking density) nitajaribu kuelezea namna moja wapo ambayo nimeiona kuwa inafaa.

Kwanza tutambue mambo ambayo yanayokupelekea kwa mabwawa mawili yenye ukubwa sawa kutofautiana idadi ya vifaranga. Ndiyo, mabwawa yenye ukubwa sawa yanaweza kutofautiana idadi ya vifaranga. SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA KUTOFAUTIANA KWA IDADI YA VIFARANGA NI KAMA ZIFUATAVYO:

I. Aina ya mfumo wa ufugaji.

Katika ufugaji samaki kuna
A) Ufugaji wa samaki peke yake bila kuchanganya na shughuli nyingine kama ufugaji wa kuku au ng’ombe na ufugaji wa samaki wenye kuchanganya na shughuli nyingine kama ufugaji wa kuku au ng’ombe katika eneo moja.

Tafiti zimeonesha kwamba ufugaji wa samaki ukichanganywa na ufugaji labda wa kuku ambapo kinyesi cha kuku kinatumika kuongeza uzalishaji wa chakula cha asili ndani ya bwawa la samaki kunapelekea kuweza kuongeza idadi ya samaki wanaoweza kufugwa katika bwawa ukilinganisha na ufugaji usiochanganya mifugo.

B) Ufugaji wa samaki kulingana na malengo ya mfugaji yaani mfugaji amekusudia kufanya ufugaji wa biashara au wahali ya kawaida tu. Maamuzi haya yataathiri mtazamo na jitihada za mfugaji katika kuliendesha bwawa lake husisani katika suala zima la CHAKULA. Kwa ujumla hapa kuna namna tatu za ufigaji samaki nazo ni

*Ufugaji wa kawaida (subsistence farming or extensive farming)
Ufugaji huu unasifa kubwa moja nayo ni kuwaacha samaki wategemee CHAKULA CHA ASILI kwenye bwawa. Kutokana na upatikanaji wa chakula cha asili kuwa mgumu kwenye bwawa, aina hii ya ufugaji humuwezesha mfugaji kufuga samaki wachache sana kutoka na uhaba wa chakula na mara nyingi samaki huitaji muda mwingi kukua ndani ya bwawa.
Ufugaji huu unamruhusu mkulima kufuga samaki 3 KWA KILA MITA MOJA YA MRABA au chini ya hapo kulingana na uwezo wa bwawa kutengeneza chakula cha asili. Pia ufugaji huu huwa hauna tija kubwa kwa mfugaji

*Ufugaji wa kiwango cha kati ( semi-extensive or semi-intensive farming )
Aina hii ya ufugaji ni ile ambayo mfugaji anajishughulisha kuwapatia samaki chakula cha ziada (supplementary feed). Kwahyo hapa samaki watakuwa wanakula chakula cha asili kinachozalishwa kwenye bwawa na chakula cha ziada anachowapa mfugaji hivyo kupelekea samaki kukua kwa haraka zaidi kuliko kasi ya ukuaji katika ufugaji wa kawaida. Ufugaji huu pelekea kuongezeka kwa uwezo wa bwawa wa kukuza vifaranga mpaka kufikia kati ya VIFARANGA 4-7 KWA KILA MITA MOJA YA MRABA ya bwawa. Ufugaji huu unakuwa na tija ya wastani kwa mfugaji.

*Ufugaji wa kiwango cha juu (intensive farming)
Ufugaji huu unasifa moja kuu ambayo utegemezi wa samaki wa mahitaji yao yote ya chakula kutoka kwa mfugaji. Aina hii ya ufugaji hutumia pesa nyingi sana kuwekeza ili kuleta faida kubwa zaidi (unmatched investment for unmatched production). Teknolojia inayo tumika hapa pia huwa ni kubwa sana. Samaki huwa wanalishwa chakula chenye virutubisho vingi zaidi ili kuwafanya wakue ndani ya muda mfupi zaidi.
Aina hii ya ufugaji inatija kubwa sana kwa mfugaji na humuwezesha mfugaji kuwa na uhakika wakusambaza samaki mwaka mzima. IDADI YA VIFARANGA HUZIDI 8 KWA KILA MITA MOJA YA MRABA.

C) Ufugaji wa samaki wa aina moja (monoculture) na ufugaji wa samaki mchanganyiko (polyculture)
Ufugaji wa samaki aina ya Tilapia kama sato unachangamoto kubwa moja ya samaki kuzaliana kwa wingi kwenye bwawa hivyo kupelekea samaki kuzidi uwezo wa bwawa wa kukuza samaki hali hii hupelekea samaki kudumaa au kuchukua muda mwingi sana kukua kifikia kiwango cha sokoni (market size) kwahyo njia mbadala huwa kufanya ufugaji mchanganyiko ambapo tilapia na kambale huchanganywa kwenye bwawa moja. Kwa kawaida bwawa huanza kwa kuwekwa tilapia kisha baada ya yakriban mwezi mmoja na nusu huongezewa vifaranga vya kambare (catfish)

Leave a Reply