JINSI YA KUTENGENEZA BUSTANI NDOGO YA NYUMBANI

Kuna njia mbali mbali waweza kuepuka kutumia mboga mboga zinazolimwa usikokujua na kuepuka kujiingiza katika afya mbaya kwa matumizi ya kemikali za kuulia wadudu na magonjwa zinazotumika katika ukuzaji wa mboga mboga.

Aina za bustani

1. Unawezatumia makopo amabayo mala nyingi hutumika kupata maua kando kando ya nyumba
2. Unaweza tumia gunia la kubwa..
3. Unaweza tengeneza key hole garden ( bustani ya tundu la Ufunguo)

BUSTANI YA MAKOPO/NDOO

Vifaa

Udongo, makopo/ndoo, mchanga/Pumba za mpunga (Rice husk), Mbole ya samadi iliooza vizuri.

Udongo – Kwa ajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia virutubisho mmea
Mchanga/Rice husk – Kusaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia kuweka mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na hewa.
Mbolea ya samadi – Kutoa virutubisho kwa mmea
 
Hatua za utengenezaji.
– Changanya udongo wako na mchanga/rice husk pamoja na mbole katika uwiano wa 5:2:1.
   5 udongo, 2 samadi, 1 Mchanga/rice husk
– Toboa makopo yako kwa chini ili kuzuia maji kubaki kwa wingi kwenye kupo na weka pamba kwenye matundu uliotoboa.
– Weka udongo uliochanganywa vizur kwenye makapo/ndoo. Hapo utakuwa tayar kupanda mbegu zako ama mche wa mboga aina yoyote.
 – Kuepuka uchafuzi wa mazingira kwa maji yanayo toka kwenye makopo endapo makopo hayo yapo kwene simenti, weka makopo/ndoo hayo juu sahani/beseni.

Uangalizi.
– Mwagilia mboga yako mala baada tu ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga.
– Unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa mboga unaweza tumia dawa zisizo za kikemikali za viwandani kama vile  majani ya pilipili kichaa, mwarobaini na tumbaku.
– Mboga kama sukuma wiki waweza vuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu.
– unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda mfano. baada ya mavuno 2 ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.. ( Hii inategemeana ni aina gani ya mboga)
Faida
– Inapunguza utumiaji wa kemikali za viwandani

– Gharama za uhitaji wa mboga za majani

SORCE:gpangetz.blogspot.com

Leave a Reply