KAHAWA NI MALI.

Na ndg.Dagras, Mwamlima.

Mwanafunzi chuo kikuu cha kilimo sokoine(SUA).

Bsc.Agricultural Economics and Agribusiness.

KAHAWA, ni zao kubwa la biashara, inachukua nafasi ya pili kwa  kuingizia taifa fedha nyingi za kigeni baada ya zao la Tumbaku, wakulima wengi wanaofuata kanuni na mbinu za kitaalam wananufaika, wanaboresha maisha yao kupitia kilimo bora cha Kahawa.

Kilimo bora kinaleta faraja

MBUSH,MWINGA Na NSALU ni wanawake wajane wa familia moja ya Mzee Nsuliho mwanahandazi kutoka kijiji cha insani ni wanachama wa kikundi cha *nswaswa* AMCOS katika kata ya Itaka wilaya ya Mbozi nyanda za juu kusini Magharibi mwa Tanzania

 

Kwa sasa sehemu kubwa ya maisha yao yanategemea Kahawa, shirika HRNS (Hanns R. Neumann Stiftung Africa linasaidia kuendeleza zao la Kahawa nchini Tanzania ili kuinua hali ya maisha ya wakulima na familia zao.

 

” Na hii ndiyo furaha ya maisha yangu” Mwinga Hazole Mwahandazi mkazi wa kijiji cha Insani,Mbozi

 

Ndio maana wanawake hao wanasema “ tunapata faida kuliko mara ya kwanza, kwa miti michache tunapata hadi zaidi ya kilo 300 za Kahawa, hii nikutokana na mbinu bora zilizotuongezea ujuzi wenye tija ya uzalishaji, tunazo jifunza kwa HRNS,pia   *one acre** **fund* wameonesha nia ya kutusaidia kulima Na kuanda KAHAWA kitalaam  maana wameshafika hapa kijijini Na ndg .zakayo Mwashibanda ndiye wakala kwa upande Wa huku kwetu”

 

“Hakika kupitia Kahawa nyumba nzuri zimejengwa, watoto wanasoma pia nimenunua mashamba mengine kwa ajili ya mazao ya chakula niweze pia kulima mahindi,maharagwe viazi mbatata ( **ndoro* )viazi mviringo ( *ntolofanyi*),parachichi,migomba Na mazao ya bustani kwenye vijito vya hapa Na pale( *horticultural* *products*)nk. kwa sasa nina shauku ya kununua usafiri wangu hasa gari”, aliongea kwa furaha Nsalu *mbwiga* mwahapumba.

“Utunzaji mzuri unaleta mavuno mengi”,Mbushi ntunyule mwahandazi.

Meneja wa mradi wa shirika la HRNS  nyanda za juu kusini, Webster Miyanda amesema HRNS linaendelea na jitihada za utafiti wa hali ya hewa ya eneo la kilimo cha Kahawa ili kutafuta suluhisho la maji “kutokana Na mvua zinazosumbua pindi muda Wa maua ya KAHAWA kuchanua ukifika hivyo kupelekea kuharibika au kuungua kwa jua kali kutoa vitendea kazi, elimu na mbinu chanya za kilimobiashara.hii itakuwa vizuri Na rahisi maana sisi kilimosmart  ndo vitu tuvifanyavyo kwa wakulima Na wale wanaotaka kujikita kwenye sekta hii ya kilimo ….kwa hayo maelezo juu _kilimosmart_  pia tunahuska Na kutoa bei za mazao mbalimbali Na masoko,mbinu nzuri za kiagronomia, viua tilifu ,thamani ya mazao katika mnyororo Wa thamani kama kubadili mwonekano ,kujitofautisha kwa bidhaa Na vifungashio bora Na safi (branding &package),kuongeza muda Na flavour kwa bidhaa Na urahisi Wa upatikanaji kwa mlaji

 

“Tunaendesha mafunzo kwa shirikisha wadau wengine kutoka kwenye mashirika tofauti yakiwemo TACRI,CMs,viwanda vya kukoboa KAHAWA kama vile Mbozi coffee curing company (MCCCo ltd),city coffee iyunga,GDM vinasaidia kutoa elimu kwa wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi”

 

 

Baadhi ya mimea inayo saidia kurutubisha udongo shambani (matandazo)

 

Lazima watumie mbinu mpya kama kilimo hifadhi, kupanda miti ya kimvuli na mazao yanayofunika udongo ndani ya mashamba ya Kahawa, pia matumizi ya mbolea ya samadi au mboji na kupanda mimea inayoongeza viini lishe vya udongo ni muhimu “alisema ndg.miyanda

UKIFUATA MBINU BORA ZA KIAGRONOMIA (KILIMOSMART APP)

Edmond Zani ni meneja wa bodi ya Kahawa kanda ya nyanda za juu kusini, amesema kwa Tanzania ikiwa mche wa kahawa utatunzwa vizuri una uwezo wa kuzalisha hadi kilogram 8  za kahawa na takribani kaya 450,000 zinategemea kilimo cha zao la KAHAWA kwa ukanda  huu hususani kata ya Itaka Na zile za jirani ikiwemo halungu Na Nambinzo hasa kijiji cha isenzanya

Acknowledged Amilisha ,Tacri,Mcco,HRNS as the source of information in facilitating this  useful piece of word for farmers and potential farmers kilimosmart app do recognise your role

@kilimosmartapp

Leave a Reply