KILIMO BILA UDONGO NA FAIDA ZAKE(HYDROPONIC SYSTEM)

hydroponic ni moja ya njia za kulima bila udongo ambapo mimea hukua kwenye mabomba au channels maalumu ambazo zinapitisha virutubisho vya mimea vikiwa kwenye maji ambavyo huenda moja kwa moja kwenye mizizi ya mimea.
FAIDA ZA KULIMA BILA UDONGO
1. Gharama za kutengeneza mfumo sio kubwa pia mfumo huu unatumika kwa miaka mingi.
2. Maji yanazunguka, kwa hiyo hayatuami.
3. unaweza kutumia media yoyote kushikia mimea kama coco peat
4. Unaweza kutumia maji hayo hayo mara nyingi. Maji yanayotoka kwenye mimea yanarudi kwenye tank yanazunguka tena kwenye mimea. Hii inapunguza gharama za maji na virutubisho vya mimea
5. Maji hayawezi kuziba mfumo.
6. Unaweza kulima bila kutumia kemikali zozote (Organic).
7. Unaweza kulima mwaka mzima bila kujali msimu.
8. Unaweza kutumia eneo Dogo kulima mazao mengi sana.

HASARA
1. Ph inabadilika kwa hiyo inahitaji ufatiliaji
2. Pump ikiharibika mimea inaweza kufa au ufanye kumwagilia kwa mkono (passive system)

source:web.facebook.com/AGRIBusinessTz

Leave a Reply