kilimo Bora cha Matango (cucumber) na mavuno kwa ekari moja

Matango (cucumber) ni zao muhimu katika mazao ya mboga na matunda nchini Tanzania na hata nje ya Tanzania.
Hili ni zao la biashara, pia chakula. Zao hili hustawi na kulimwa kwa wingi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Pwani.
Matumizi: Matango hutumika kama tunda, ijapokuwa ni aina ya mboga na huongeza vitamin A, C na maji mwilini. Pia, tango linaweza kutumiwa kama saladi wakati wa mlo.

Hali ya hewa: Matango hustawi kwenye hali ya joto, hali kadhali kwenye sehemu yenye joto kidogo pia hustawi. Matango yanahitaji joto wastani wa nyuzi joto 20°C – 25°C. Zao hili pia huhitaji maji kwa wingi, ingawa unyevu ukizidi husababisha magonjwa kwenye majani na maua.
Udongo: Kwa ustawi mzuri wa matango,
udongo unatakiwa kuwa na rutuba ya kutosha, na chachu ya kuanzia 5.5 hadi 6.7, mwinuko unaotakiwa ni kuanzia mita 1000-1200 kutoka usawa wa bahari.
Tofauti na ilivyo mazao mengine, matango hayahitaji mwanga mkali sana kwa kuwa husababisha maua dume kuzaliwa, hivyo kuathiri uzalishaji wa idadi ya matunda ya matango. Mwanga kidogo husababisha maua jike kuchanua kwa wingi kuongeza kiwango cha mazao. Mwanga unapokuwa mwingi, inabidi kutumia neti au aina nyingine ya vizuizi ili kupunguza mwanga, ambapo pia itasaidia kulinda mmea dhidi ya upepo mkali ambao unaweza kuharibu maua na matunda, au mmea kwa ujumla.
Kupanda: Mara nyingi matango hupandwa moja kwa moja shambani. Wakulima wengine hupanda kwenye vitalu au makopo na baadae kuhamishia miche inapofikia sentimita 8-12. Endapo mbegu zimepandwa shambani moja kwa moja, inatakiwa ipunguzwe na kubakia mche mmoja tu kwenye kila shimo.
Nafasi: Nafasi kati ya mche na mche ni sentimita 60-70, na nafasi kati mstari na
mstari ni sentimita 70-90. Mimea inatakiwa
iwekewe miti ili iweze kuzaa matunda mengi na kuepuka kukaa chini ambapo matunda yanaweza kuoza au kuharibiwa na wadudu.
Mbolea: Mbolea ni muhimu sana, kabla ya
kupanda au kuhamisha miche. Mbolea
inayoweza kutumika ni samadi au ya
viwandani isiyokuwa na madhara kwa
mazingira na afya ya binadamu. Baada ya kupanda, tumia mbolea ya maji maji kila baada ya siku 14-21, mpaka mmea uweke matunda.
Palizi: Palizi ni muhimu , ili kuepuka magonjwa na kunyang’anyana chakula kati ya zao na magugu.
Wadudu waharibifu: Wadudu waharibifu wa matango ni pamoja na Vidukari, inzi weupe, na minyoo ya mizizi.
Magonjwa: Magonjwa yaliyozoeleka kushambulia matango ni pamoja na Ukungu, fusari, na magonjwa ya virusi.
Kuvuna: Matango yanaweza kuwa tayari kuvunwa kuanzia siku 50-60 na matunda yanatakiwa yawe na urefu wa sentimita 15 mpaka 20. Makadirio ya mavuno ni tani 6 kwa ekari moja.****Na.2: Ugonjwa wa Umasikini Akili yako ****

KILIMO CHA MATANGO Kinakutoa,

Kijana angalia hii hesabu ndogo kabisaa Lima ekari moja iliyopandwa na kustawi vizuri inaweza kuzalisha viroba 130 hadi 150 vya ndoo tatu za Lita 20. Hivyo kwa ekari mmoja unaweza mfano chukua 130 ukauza bei ya hovyo kabisaa @70,000/ x130 = 9,100,000/= kwa hiyo ekari moja. Jamani ndani ya Siku 45 – 50 unapata pesa hizi ambapo hata kama utatumia 1M kuzalisha bado una faida tu.

Je,Unataka nini Tanzania Maji yako Ardhi IPO nani Masikini kama si Akili yako? Tunaleta mjadala hii kubadili fikra zetu juu ya Kilimo hata kama masoko changamoto badili kuwa fursa sasa.KILIMO CHA MATANGO.
Tunda linalostawi maeneo ya kitropiki na lenye faida kemkem za kiafya ikiwemo upatikanaji na vitamin A pamoja na waswahili husema ulaji wa tunda hili husafisha figo, na huku wataalamu wakieleza tunda hili Husaidia katika kuongeza maji mwilini, pia Husaidia katika mmeng`enyo wa chakula.

Mikoa mingi hapa Tanzania huzalisha zao hili kwa wingi, ikiwemo Arusha, Tanga, Tabora, Mwanza, Pwani, Morogoro na mingine mingi.

HALI YA HEWA.
Joto liwe 18 hadi 35 setrigrade, mvua iliyo ya wastani, umbali kutoka usawa wa bahari ni mita 1000 – 1200.mvua ziwe za wastani.

kwa kilimo cha matango suala la kuzingatia ni kuhakikisha unapanda mbegu bora na unafuata kanuni zingine za kilimo, ikiwemo kuzingatia uandaaji wa shamba kwa kusafisha na kuondoa kila aina ya uchafu uliopo pia kuandaa matuta yenye muinuko na kuweka mashimo katika vipimo vinavyotakiwa, upandaji wa nafasi, palizi, uzuaji wadudu wasumbufu kama inzi weupe, usegekaji (staking), kuvuna kwa wakati. Usipande matango sehemu zenye mwanga mkali au sehemu ambazo zenye kivuli, hivyo matango yapandwe katika sehemu zenye mwanga wa kutosha na sio uliozidi au kupungua, kwa kuzidi kwa mwanga matango hupelekea maua dume kuzaliwa kwa wingi, na kwa kupanda sehemu zisizo za mwanga hupelekea maua ya kike kuzaliwa kwa wingi, pia ukuaji duni pamoja na magonjwa ya fangasi.

Hili kuziia mwanga kuzidi au kupungua kilimo cha greenhouse kimefanikisha hili suala la mwanga, mbali na hapo waweza tumia nailoni maalumu kwa suala la mwanga.

MAANDALIZI YA SHAMBA.
Kabla ya kuandaa shamba chagua sehemu ya kuweka shamba lako la matango, shamba liwe na udongo tifutifu udongo ambao unapitisha maji, udongo wenye rutuba, wenye chachu ya udongo (soil pH) 5.5 hadi 6.5. sehemu pia mzungo wa hewa uwe wa kutosha.
Shamba liwe sehemu inayofikika kwa urahisi pamoja na hayo shamba liwe karibu na barabara kuu ambayo itarahisiha usafifrishaji kutoka shambani kwenda sokoni.

USEGEKAJI (STAKING).
Weka miti (nguzo) katika kila shimo lenye mche kwa lengo la kuuweka mmea kuwa imara na matunda kuwa yenye ubora kwa kuacha matunda kuwa chini hupelekea matunda kuoza na wadudu kutoboa.
Miti hii iwekwe ikiwa na mtindo wa matawi na usiwe mti wenye kunyooka kama inavyotumika katika nyanya.

AINA ZA MATANGO.
Zipo aina nyingi za matango ambazo huzalishwa hapa nchini zikiwemo, Colorad, Telegraph, Palmetto, Chicago, Pickling, Straight 8 na Marketer.

UPANDAJI.
– Ni vizuri ukapanda mbegu za matango moja kwa moja shambani na huchukua muda wa siku saba.
– Japo wakulima wengine hupendelea kupanda kwenye vitalu kwanza na baadae kupeleka katika shamba kuu na miche ya matango huamishwa unapofikia urefu wa sentimeta 8 hadi 12.
– Matango hustawi zaidi katika udongo wenye rutuba na unaopitisha maji hapa udongo ni muhimu huwa wa tifutifu.
– Kina cha upandaji ni mita 30.
– Panda mbegu moja katika kila shimo moja.

NAFASI ZA UPANDAJI.
Nafasi kati ya mche na mche nii sentimeta 60 – 70 nafasi kati ya mstari na mstari ni 70 – 90

MATUMIZI YA MBOLEA.
Kwa udongo usiokuwa na rutuba ya kutosha uwekaji wa mbolea ni jambo la msingi kuhakikisha unapata mmea wenye afya.
Kabla ya upandaji andaa shamba lako kwa kuweka mashimo ambayo yatawezesha ukuaji mzuri wa mmea.
Weka samadi itokanayo na wanyama kama ng’ombe, kuku, mbuzi cha kuzingatia mbolea iwe imepoa zaidi ya wiki moja na zaidi, na isiwe ya moto yapaswa kuwa imekaa zaidi ya wiki.
Kwa kutumia mbolea za viwandani (mbolea za chimvi chumvi), tumia mbolea aina ya DAP, NPK. Kwa kupandia tumia mbolea ya NPK na kwa kukuzia tumia DAP.

WADUDU WAHARIBIFU
Wadudu waharibifu katika matango ni
– Inzi weupe (fly fruit).
Wadudu hawa hukaa chini ya majani ya mmea.
Na husababisha majani kusinyaa na kuwa namikunjo.
– Minyoo ya mizizi (nematodes).
Minyoo hii hupeleka kudumaa kwa mmea, minyoo hii huonekana kwa mafundo kwenye mizizi.
– Cucumber Beetle (Tango mende).
Huyu ni mdudu mbaya sana kwa zao hili. Hutafuna miche ya matango na maboga mara ichipuapo, pia hushambulia majani ya mimea michanga
– Melon Aphid.
Hufyonza utomvu wa mimea. Tumia Malathion. Hakisha dawa inafikia upande wa chini wa majani
– Funza.
Buu au funza hujipenyeza ndani ya ua,kisha huhamia kwenye tunda.Tumia Rotenone au Crylite kila baada ya jumla.

MAGONJWA
– Magonjwa ya bacteria.
Majani yaliyoshambuliwa hunyong’onyea na kudhoofu na hatimaye hufa. Mmea ukikatwa huchuruzika ute mzito. Nyunyizia dawa ya Copper kila baada ya siku 10 na tumia aina zenye uvumilivu mkubwa kama vile Palmetto.
– Ubwiri poda (Powdery Mildew).
Ukungu wake hushambulia majani na mashina. Nyunyizia dawa ya unga ya sulphur kila baada ya siku 10.
– Virusi vya wadudu (Cucumber Mosaic)
Husababishwa na sumu (virus). Hali ikiwa mbaya zaidi mmea hugeuka njano, hudumaa na hushindwa kutoa matunda. Huenezwa na magugu au wadudu kama aphids na beetles. Usafi bustanini unahitajika.

– Ukungu (Fog)
Ugonjwa huu husababishwa na hali ya hewa ya ubaridi, na namna ya kuuziana ugonjwa huu ni matumizi ya dawa/sumu maalumu ambazo ni copper fungicide.
– Magonjwa ya virusi (viral disease).
Sehemu athirika ni majani, shina pia huathiri ukuaji wa mmea.
Magonjwa mengi ya virusi huzuiliwa na kupanda mbegu ambazo zinahimili magonjwa.
– Kuoza kwa matunda (Fruit rot)
Kuoza kwa matunda hutokea pale ambapo hutaruhusu matango kutambaa chini na wadudu kushambulia matango kwa urahisi, hivyo uwekaji wa miti katika mashina ya matango kuoza huku kutaepukika.

MATUMIZI YA VIATILIFU.
– Matumizi ya viatilifu yategemee sana hali ya mmea kama imeshambuliwa na magonjwa au wadudu,
– Matumizi ya viatilifu/dawa/sumu kulingana na ushauri wa wataalamu.

KUVUNA
Matango huchukua siku 50 hadi 60 shambani hadi kuwa tayari kuvunwa na matunda yanakuwa na urefu wa sentimeta 15 mpaka 20, makadirio ya mavuno ni Tani 6 kwa ekari moja.

MAMBO YA KUZINGATIA.
Panda kwa wakati, hakikisha unachanzo cha maji ambacho hakita tegemea sana mvua, zuia magugu na magonjwa hii itapelekea mazao yako shambani uwa na uhakika wa kuvuna na kupata faida uanayo itegemea.
Mara baada ya kuvuna kwa wakati hakikisha una osha baada ya kuvuna hili kutoa joto ambalo limetokanalo shamba.
Usipulize dawa/sumu yeyote endapo muda wa kuvuna umekaribia na kama utakuwa umepulizia hakikisha kuwa muda wake mpaka dawa ile hiishe ndio unavuna usipeleke mazao ambayo yana mabaki sumu kwani utahumiza watumiaji wa matunda haya.
Muda unaoshauriwa kuvuna mazao yako ni iwe mapema asubuhi au jioni ya kuanzia saa kumi mpaka pale jua litakapo zama, lengo la kufanya hivi ni kuepuka jua kali kwani upelekea kuharibu ubora wa mazao baada ya kuvuna.
Kwa wanao safirisha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ambayo ni umbali mrefu usisafirishe wakati wa jua kali safirisha muda ambao ni tulivu na hakuna joto kali au kusafirisha wakati wa usiku, hii itasaidia kuwa na mazao yenye ubora unaoitajika sokoni.
Hakikisha unapeleka mazao yenye ubora na ukubwa kwa lengo la kupata faida nzuri.Kilimo cha matango kilimo cha muda mfupi sana kinaweza kuchukua hadi siku 45 tu kuanza kupata zao la Kwanza la kuuza. Na mpaka imalize kuchuma unaweza kupata michumo mitano hadi nane.Kuna matango pori, kisasa nayo kuna aina tofauti. ..kuna lazima uning’inize, uweke miti. .mingine yanatambaa tu kama kienyeji

source: Kilimo CHA Kisasa ZAIDI

 

Leave a Reply