KILIMO BORA CHA NYANYA (1)

UTANGULIZI 

Nyanya ni aina ya mboga inayo zalishwa kwa wingi sana duniani. Kwa Tanzania, nyanya ni zao la kwanza katika mazao ya mboga linalo limwa na kuliwa kwa wingi ukilinganisha na mboga zingine. Nyanya hutumika karibu Katika kila mlo. Nyanya ni jamii ya mazao ya Solanaceae, mazao mengine marufu katika kundi hili ni pilipili hoho, biringanya, ngogwe na viazi mviringo. Uzalishaji wa nyanya unahitaji uangalizi na matunzo ya hali ya juu katika huduma ya pembejeo. Pamoja na hayo zao hili linaweza kumpatia mkulima faida kutokana na mahitaji yake katika matumizi ya kila siku kwenye familia za aina zote.

Hali ya hewa

Nyanya hustawi vizuri kwenye hali ya hewa yenye joto la wastani kati ya nyuzi joto 21 na 32 C na katika mwinuko  wa mita 300-1400 juu ya usawa wa bahari na huhitaji maji mengi kiasi cha mm 1800 kwa msimu.

Udongo

Udongo tifutifu wenye rutuba ya kutosha usiotuamisha maji hufaa zaidi kwa kilimo cha nyanya, japo kuna uwezekano wa nyanya kuzalishwa hata katika udongo wenye kichanga au mfinyanzi. Kiwango cha tindikali na nyongo katika udongo ( Soil pH) kinapaswa kudhibitiwa. Nyanya hustawi vizuri kwenye tindikali ya 6-6.5 (Soil pH)

Aina za nyanya 

Kuna aina kuu mbili za nyanya

Nyanya zinazokuwa ndefu (Indeterminate)

Aina hii ya nyanya huendelea kukua na kuzaa kwa muda mrefu. Hutolewa machipukizi au maotea na kubaki shina moja au matawi mawili tu. Husegekwa kwa kutumia miti mirefu, kamba ndefu na wakati mwingine nyaya hutumika.Nyanya aina hii na mahususi kwa kilimo katika mabanda (greenhouse). Mkulima anaweza kulima aina hii ya nyanya nje lakini ana hitaji kuwa na nguvu kazi kubwa. Ukiilima ndani unaweza vuna kwa muda usiopungua miezi 9 na iwapo utailima nje unaweza vuna kwa muda usiopungua miezi 4 mfululizo.Mfano wa mbegu hii ni ; Anna F1, Tylka F1, Eva F1, nk.

Nyanya ndefu katika banda ( green house)

Nyanya fupi ( Determinate)

Hizi ni nyanya fupi, zinakuwa na kikomo cha kukua ndani ya muda mfupi. Huvunwa kwa muda mfupi, kiasi cha miezi 2-3 tu.Ni nyanya zinazoshauriwa kulimi na kibiashara na wakulima wenye mashamba makubwa.  Aina hii ya nyanya aipogolwei machipukizi na huwekewa miti mifupi ya kiasi cha mita 1.5. Mfano wa aina hii ya mbegu ni Kilele F1, Asila F1, Edeni F1, Nuru F1, Monica F1, Jara F1, Tanya, Mwanga, Riogrand, nk.

NB: Aina hizo mbili za nyanya pia zimegawanyika; kuna mbegu chotara (Hybrid) na mbegu zilizoboreshwa (OPV) na mbegu chotora ndio mbegu nzuri zaidi.

Mfano wa mbegu chotara (Hybrid) ni;

Asila f1, Anna F1, Kilele F1, Edeni F1, Nuru F1, Rambo F1, Monica F1, Milele F1, Jara F1, Tylka F1, Kipato F1, Shanty F1, nk

Mfano wa mbegu za kawaida zilizoboreshwa ni; Tanya, Rio Grande, Onyx, Tengeru 97, Mwanga, nk

Mahitaji ya mbegu.

Ni muhimu kutumia mbegu bora kila wakati. Kiasi cha gramu 50-100 ya mbegu hutosha kupanda ekari moja kutegemea njia usiaji, uotaji na nafasi ya kupanda. Mbegu ya nyanya huota baada ya siku 4-8.

kilimo smart

Nyanya Fupi, nanenane, 2014- Morogoro Tz.

Kusia/vitaru.

Kuna aina mbili kuu ya vitaru, vitaru sinia ( Tray) na vitaru vya chini. Vitaru sinia ni vizuri sana kwani husaidia kuepuk magonjwa ya ardhini na ukitunzia miche ya kwenye vitaru sinia miche hukua vizuri na kwa haraka zaidi.

Vitaru vya chini pia vimegawanyika, kuna vitaru mbinuko na vitaru mbonyeo. Vitaru mbinuko ni vizuri kwani husaidia hewa kuzunguka kwa urahisi.

Kwa kawida miche nyanya huwa tayari kupandikizwa shamba kubwa baada ya siku 21 tangia kumwaga mbegu chini/kusia.

Imeandaliwa na Agronomist Peter 0623642293

Leave a Reply