Kilimo cha HoHo


Nianze na Kusisitiza kuwa kilimo Kinaanzia Sokoni fanya tafit zako vyema kabisa kabla hujaamua kulima jua wateja wako, jua msimu ambao hoho hukusekana na jua bei za hoho kwa kila msimu,

Kilimo cha pipipili Hoho ni kama Kilimo cha mazao mengine ya bustani kama nyanya, tikiti, etc
Katika Kilimo hichi kuna mambo kadha wakadha ya kuzingatia

  1. KITARU
    Unatakiwa kuandaa kitaru kwa umakini, unahakikisha umelainisha udongo, ili uwe tifutifu, kabla hujapanda unashauriwa kupiga dawa ya fungicide ili kuzibiti magonjwa kwenye udongo KITARU ni sehemu ya kuzingatia sana, katika upandaji wa mbegu zozote, za bustani na ni vyema kutandaza nyasi juu ya KITARU ili kuwepo na unyevu wakotosha ili kulahisisha mbegu kuota vizuri, mbegu za Hoho kutumia siku 8-10 kuota hivyo ni vyema kuzingatia kuweka nyasi na kumwagilia maji ya kutosha

2.MBEGU ZA HOHO

Katika Kilimo cha Hoho kuna kampuni mbali mbali huuza mbegu za Hoho lakini mbegu hizi pia hutofautia kuhimili magonjwa na kuwa na mavuno mengi , vile vile katika zao hili kuna mbegu zinakuwa na marunda makubwa na mengine ya wastani , hivyo ununuzi wa mbegu hizi utegemee aina ya wateja ulionao au SOKO unalotegemea kuuza
Aina nzuri ni yolowander B, na improved variety ambazo husmbazwa na kampuni ya Mkulima,

3.MAGONJWA NA DAWA ZAKE
zao la Hoho husumbuliwa na magonjwa kadhaa lakini ni vyema kuzia magonjwa kuliko kutibu magonjwa yanayosumbua ni ukungu ambapo ni vyema kupiga dawa ya ukungu, kila baada ya wiki moja , dawa hii iendelee kupigwa tangu kwenye kitaru hadi kipindi cha kuanza kuvuna dawa za ukungu ni kama vile ivory 72, linkomil 72, ambayo huzuia na kutibu iwapo zao litakuwa limepata ugonjwa tayari
Madawa mengine ya kuzuia magonjwa mengine ni kama bamic, abamectrin, banophose, Konto, farm guard, etc

KUANDAA SHAMBA ILI KUAMISHA MBEGU (TRANSPLANTING)

Ni vyema kipindi tu unapoweka kitaru uanze uandaaji wa shamba lako ili uweze kuliandaa kwa ufanisi
Katika uandaji huo itakuwemo kuandaa kwa kulima, kupiga halo, na kutengeneza matuta kabla hujapanda unashauriwa kumwagia maji Ardhi ili ipoe kama ni sehemu ya joto Kali sana ikiwemo kuchimba mashimo na kuyawekea Mbolea, zao la Hoho pia huitaji maji ya kutosha kuanzia kupanda hadi kuvuna, Mbolea iweke kulingana na ushauri wa mtalaam alie karibu na wewe,

KUHUDUMIA SHAMBA

Palizi ifanyike mara magugu yanapotokea shambani. Umwagiliaji maji ufanyike kama ilivyo kwa mazao mengine kama nyanya. Tumia mbolea kiasi cha kilo 140 za SA au CAN kwa hekta hasa wakati mmea inapotoa matunda ili kupata matunda makubwa na kuvuna kwa muda mrefu (hadi miezi 10).

MAGONJWA NA WADUDU (hii ni Maendelezo wa Part ya Magonjwa

Wadudu
• Funza wa vitumba
• Vidukari
• Kidomozi (Leaf miner)

Kudhibiti: Tumia dawa aina ya permethrin
Magonjwa
• Kuoza mizizi
• Mnyauko wa majani
• Batobato
Kudhibiti: Choma nyasi kwenye kitalu kabla ya kusia mbegu.
Badilisha mazao yasiyo ya jamii ya pilipili.

UVUNAJI

Matunda ya kwanza huwa tayari kuvunwa kuanzia miezi 2-3 baada ya kupandikizwa; matunda yaliyokomaa vizuri na kuwa na rangi nyekundu ndiyo huvunwa. Matunda 30-80 hupatikana kwa mmea mmoja.
Ubora wa hoho huongezeka kutegemeana na kiwango cha rangi yake ikiwa ni nyekundu njano au kijani. Mazao kiasi cha tani 3.5 kwa hekta hupatikana. Baada ya kuvuna mwagilia maji, piga dawa (kama ni muhimu) na weka mbolea kuongeza uzalishaji unaofuata.

GHARAMA YA UZALISHAJI WA HEKTA MOJA*

Mbegu Tshs. 48,000 /-
Vibarua 520,000/-
Mbolea(mboji/samadi) 500,000/-
Madawa 120,000/-
Jumla 1,620,000/-

MAPATO
Ndoo Moja Kipindi cha msimu Mbaya ni, 5,000 na Kwa heka moja unaweuzao wa Kuvuna Gunia 7 kila wiki, ambao ni ndoo 42 X4 X 5 month productive harvesting=4,200,000

Potential harvest ndoo 70 /Week 4X 8000×5/ Reasonable price mapato 11,200,000

NB MAPATO HUTEGEMEA MSIMU NA BEI YA SOKONI

By Otaigo +62 852-1786-7577

Leave a Reply