Kilimo cha nyanya-uandaaji shamba (2)

Maandalizi ya shamba

Lima shamba kwa kina cha sentimita 30-45 na kisha andaa matuta yenye upana wa sentimita 150 kutoka katikati ya tuta moja na lingine.Unaweza lima bila matuta lakini zipo faida zitokanazo na matumizi ya matuta katika kilimo, baadhi ya faida hizo ni kuwa matuta huweza kuruhusu mizizi kusambaa vema na kupata virutubisho, unyevu na hewa. Matuta pia huondoa maji mengi yaliyozidi shambani hasa wakati wa mvua nyingi.

Upandaji.

Nyanya hupandwa kwa umbali wa nafasi ya sentimita 30 mche na mche na sentimita 60 mstari na mstari ( kwa mbegu za kawaida zilizoboreshwa). Kwa mbegu chotara inshauriwa mche na mche iwe sentimita 60 na mstari na mstari iwe sentimita 90.  

Panda kwa kutumia mbolea kianzio (starter solution), tengeneza mwenyewe hiyo mbolea kwa kutumi DAP ( Tutajifunza kwa vitendo shambani)

Uwekaji miti /usegekaji

Nyanya ni mimea nyenye shina laini lisiloweza kusimama wima bila usaidizi, hivyo basi ili kuweza kuongeza uzalishaji kwa kuepuka magonjwa ni muhimu mimea nya nyanya iweze kuwekewa miti ili isimame imara bila kutambaa ardhini. Zipo aina nyingi za uwekaji miti kutegemea na aina ya nyanya, kama ni fupi au ndefu na pia hutegemea na upatikanaji wa vifaa kama vile miti, fito, waya, nk.

Uwekaji miti hupunguza mashambuzi ya magonjwa na wadudu kwa kuruhusu mzunguko wa hewa kupita vema na kuongeza ukuaji mzuri kwa kuruhusu mwanga na kupenya kwa urahisi.

Kupunguza machipukizi/ Maotea na majani

Ni muhimu kwa nyanya ndefu kuondoa machipukizi na kabakia shina moja ili kupunguza msongamano na hivyo mimea huzaa matunda yenye ubora wa kutosha. Kwa nyanya fupi hakuna sababu ya kupunguzia. Majani hupunguzwa matunda yanapokaribia kokomaa.

uamdaji wa shamba

Palizi

Magugu hushindana na mazao katika kugombea virutubisho, mwanga, hewa na unyevu. Magugu ni moja ya visumbufu kwa mazao yetu. Shambaa lililojaa magugu huvutia wadudu na vimeleavya magonjwa kuweza kujificha na kufanya mashambulizi kwa mazo hivyo shart yaondolewe na kuacha shamba likiwa katika hali ya usafi kila wakati. Zipo njia kadhaa za udhibiti wa magugu shambani, kama palizi, kung’oa kwa mkono, kutumia viuagugu na kutumia matandazo.

Imeandaliwa na Agronomist peter 0623642293

Leave a Reply