KILIMO CHA PILIPILI MBUZI


MBEGU NA JINSI YA KUSIA/KUMWAGA
Tafuta mbegu bora iliyoandaliwa kitaalamu kwa Tz unaweza pata mbegu bora ya pilipili mbuzi kutoka Kampuni ya AYEGRO Group Ltd. Mbegu 100g zinatosha kupanda ekari moja.
Andaa kitaru chako vizuri chenye ukubwa wa mita moja kwa sita ((1 x 6) m),Ili hewa iweze kuzunguka vizuri kwenye udongo unashauriwa kutengeneza kitaru mbinuko.Kama una mbolea aina ya samadi iliyooza vizuri (Well decomposed) changanya debe 3 kwenye kitaru cha mita moja kwa sita.Hakikisha unachanganya vizuri udongo na samadi hadi ushindwe kutofautisha kati ya samadi na udongo,baada ya kuchanganya samadi na udongo sasa sawazisha vizuri,hakikisha hakuna mabongemabonge.
Kama huna mbolea ya samadi tumia DAP baada kuanda kitaru chako rushia DAP kiasi cha 180g kwa kitaru cha mita moja kwa sita au kwa lugha nyingine ni 30g kwa kila square mita moja
Baada ya kuweka mbolea tengeneza mistari inayopishana kwa umbali wa sentimita 4 na baada ya hapo sia/mwaga mbegu zako kwenye hiyo mistari NB:Usibananishe mbegu wala kuziweka chini sana.
Baada ya kuweka mbegu kwenye hiyo mistari fukia vizuri kwa kutumia udongo laini na kisha tafuta majani makavu na tandika kitaru chako vizuri na baada ya hapo mwagilia maji ya kutosha kwa kutumia Keni ya kumwagilia.
Mbegu zitaota baada ya siku 7-10 na baada ya kuota toa majani na kama ni masika tengeneza kichanja na tandika juu ya kichanja,kama ni kiangazi unaweza kuacha kuweka kichanja.
Siku mbili baada ya mbegu kuota mwagilia maji ya kutosha na kisha pulizia Actara au dawa yoyote yenye kiambato sawa na Actara ( Thiamethoxam ). Pulizia dawa nyingi mpaka udongo ulowane zaidi (Drenching), pima Actara 8g/20L.
Siku 4 baada ya mbegu kuota pulizia Ridomil gold au Ivory 72 , pima 50g/20L. Baada ya siku 14 tangia upulizie Actara pulizia dawa inaitwa Cutter,pima 15ml /20L au Snowsoldier,pima 75 ml/20L, Pia siku 14 tangie upulizia Ridomil gold pulizia dawa inaitwa Score au Xantho pima 20ml/20L, lakini pia siku ya 7 tangia miche iote weka mbolea aina ya Yaramila winner kiasi.
Miche ya pilipili mbuzi hukaa kwenye kitaru siku 30-35 na baada ya hapo unahamishia shambani.
UPANDAJI.
Andaa shamba lako vizuri muonekano wa shamba utategemea njia unayotumia kumwagilia. Panda kwa kuzingatia nafasi. Kutoka mmea na mmea iwe 70 cm na mstari na mstari iwe 1m (100 cm) kulingana na aina ya mbegu).Pandia DAP 5-10g /mmea. Hakikisha mbolea haigusani na mizizi au Panda miche bila mbolea mwagilia maji na kisha tengeneza starter solutions.NB:Chukuwa kilo 3 za DAP weka kwenye maji lita 200 na kisha kologa mpaka mbolea yote iyeyuke na kisha chota kwa kutumia kikombe cha chai kidogo na mwagilia miche yako aliyopanda siku hiyo,hakikisha maji yenye mbolea hayagusi majani ya miche yako…mwagilia chini kwenye udongo tu sio majani.
MBOLEA.
Siku 10 Baada ya kupanda sasa endelea kukuzia mbolea,wakati huu tumia Yaramila winner 510g kwa mche.NB:Usitupie juu..hakikisha mbolea unaifukia kuzunguka mmea na usiweke karibu sana na mmea,weka 4-6 cm kutoka kwenye mmea.
Na baada ya siku 21 weka mbolea aina ya Yaramila winner au NPK na maua yakianza weka Yaramila nitrabo au CAN 10g /kwa mmea ,na baada ya hapo utaendelea Kwa kuchanganya Yaramila winner na CAN au yaramila nitrabo (5g yaramila winner +5 CAN=10g kwa kila mmea) na weka kila baada ya siku 28 mpaka mwisho wa mavuno ila pulizia Super grow kila baada ya siku 14 au kila baada ya kuchuma.

WADUDU Pilipili mbuzi hushambuliwa na ; A) Wadudu mafuta ( Aphids)
Kuwadhibiti.
✓ Tumia Actara 8g/20L. ✓ Au tumia wadudu wanaokula wadudu mafuta,mfano special beetles.
B) Crickets Hawa wadudu hukaa aridhini karibu na mmea na usiku hutoka walipo jificha na kukata miche michanga.
Kawadhibiti.
✓ Unapo andaa shamba andaa vizur ili nyumba zao zife na kuwaacha katka halu ya hatari ya kuliwa na ndege na wadudu wengine ,kama ni miche na iko kwenye tray…basi weka hizo tray juu ya kichanja.
C) Beetle.
✓ Tumia, Karate 40cm/20L.
D) Utitiri
✓ Dawa:Tumia Dynamec au yoyote yenye Abamectin.
E) Nematodes na nk.
✓ Tumia solvigo.
F) Vithiripi (Thrips)
✓ Tumia Snowsoldier au Cutter
MAGONJWA. 1) Fusarium wilt (Mnyauko) Njinsi ya kuepuka.
✓ Tandika shamba lako na majani makavu ili kupunguza joto. ✓ Ng’oa mimea yote iliyougua na choma moto mabaki. ✓ Epuka kusambaza ugonjwa kwa kusafisha vizur vifaa vya shamba na chini ya miguu uingiapo shambani. ✓ Jitahidi mimea iwe na afya nzuri kwa kuweka mbolea na maji ya kutosha. ✓ Pulizia dawa ya kuvu kama vile ortiva au Evito T
2) Southern blight ( Sclerotium wilt) Huu ungonjwa utaona kwenye shina china panaota fangasi weupeweupe (Whitish fungal growth on the stems of infected plant) .Majani ya chini huweza kunyauka,Huu ungonjwa hutokea muda mfupi kipindi cha joto kali.
Kuepuka/Kuzuia.
✓ Wakati wa kulima ..lima hadi chini sana ili hao fangasi waende chini sana ambapo mizizi haifiki. Mimea iliyoshambuliwa…Ing’oe yote na choma moto lakini chomea nje ya eneo la shamba na Pulizia Ortiva mimea iliyobaki.
3) Anthracnose.
Huu ni ugonjwa ni wa kawaida kwenye pilipili mbuzi na huu ugonjwa huweza kukaa ardhini muda mrefu. Dalili zake utaona matunda kama kuna sehemu yanakuwa meusi na yanajaa majimaji …dalili hii huenea sehemu kubwa ya tunda na baadaye tunda huoza.
Kuepuka.
✓ Kuepuka ugonjwa kujirudia musimu na musimu. Baada ya kuvuna choma mabaki yote. Shamba ambalo ulilima pilipili usirudie kulima pilipili mfululizo zaidi ya mara mbili…badilisha zao kwa kupanda zao ambalo sio jamii moja na pilipili mbuzi (Do crop rotation), Pia huu ugonjwa huweza kupitia mbegu…kwa hiyo mkulima lazima achukue mbegu kutoka kwa wakala aliyeidhinishwa na mwaminifu…mbegu hazitakiwi kutengenezwa kutoka kwenye mimea iliyoathirika na ugonjwa.
4) Bacteria. Madoamadoa ya bacteria kwenye matunda., huweza kutokea na kusambaa haraka wakati wa joto kali na unyevu kwenye udongo.Pia huu ugonjwa huweza kuenea kupitia mbegu.
Dalili zake utaona madoamadoa ya kama brown chini ya majini na pia kwenye matunda.
Kuepuka.
✓ Usitengeneze mbegu kutoka kwa mimea iliyoathirika na huu ugonjwa.Nunua kutoka kwa wakala. ✓ Pulizia dawa yoyote yenye copper kama vile blue copper.
5) Virusi. Kuna aina nyingi ya virusi ambao hushambulia pilipili mbuzi. Dalili zake ni majani kuwe ba njano na kujikunja .
Kuepuka.
✓ Nunua mbegu bora ✓ Pulizia dawa za wadudu kuanzia kwenye kitaru na kuendelea.Wadudu wanaosababisha virus sanasana na wadudu mafuta (thrips na Aphid) kwa hiyo akikisha muda wote shambani hakuna hao wadudu kwa kupulizia Actara,au Snowsoldier au Cutter.
NB:Pamoja na maelezo yote hapo juu.Usikae zaid ya siku 14 bila kupiga dawa ya wadudu na ukungu/fangasi hata kama hakuna ugonjwa wala wadudu.

Kwa ufupi magonjwa na wadudu wanaosumbua sana kwenye pilipili mbuzi

Picha hizo hapo juu ni madhara ya vithiripi (Thrips),dawa nzuri ni Snowsoldier na Cutter tumia dawa hizo mbili kwa kubadilisha.

Ugonjwa unaosumbua sana ni ubwiri unga na Bakteria.

Ubwiri unga-tumia Xantho au Score, au Thiovet jet au Salfarm au Cosavet 80% au Devisulphur80% WP au Anvil 5SC au Mupavil 50SC
NOTE: Nimekuandikia dawa nyingi nikiamini huwezi kosa moja wapo wa hizo karibu nawe.
Inashauriwa usipige dawa aina moja mfulilizo kuepuka usugu wa dawa,kwa hiyo ni vizuri kuchagua dawa 2 au 3 za magonjwa na wadudu pia unakuwa unabadilisha.
Mfano, mimi kwa ajili ya magonjwa natumia Xantho,blue copper na Salfarm, ratiba yangu iko hivi: Nikipiga Xantho leo baada ya siku kati ya 7-14 napiga Salfarm,halafu baada ya siku zingine 7-14 napiga blue copper kisha naanza kurudia….kwa hiyo ni mzunguko.
NB: Kwenye mzunguko wako wa dawa isikose dawa ambayo ina sulphur lakini pia dawa yenye copper isikose na inashuriwa utumie dawa aina tatu tofauti katika mzunguko.

Wadudu natumia: Snow soldier then Cutter au Abemectin then snowsoldier then cutter…sirudii dawa moja mfulilizo .NB: Ukikosa hizi dawa tafuta dawa yoyote yenye Emamectin Benzoate 21.5g/L au Carbosulfan

Bakteria -Tumia dawa yoyote yenye copper kama vile Blue copper / Cobox 50/ Cuprocaffaro 50 WP/ Tancop 50%WP/ Copper Nordox.

Mavuno.
Utaanza kuvuna baada ya siku 90 tangia uhamishie miche shambani na utaendelea kuvuna kwa muda wa miezi 6-12 kulingana na matunzo yako. Kila baada ya wiki mbili unavuna na kila ukivuna kwa ekari moja hutoa gunia 10-20 kulingana na huduma yako.
SOKO
Soko la pilipili mbuzi Tz ni kubwa sana japo kuna muda zinashuka bei lakini bado mkulima anapata faida.
Bei ikipanda sana huwa Debe ni Tsh 30 000-60 000.Hii mara nyingi hutokea miezi ya 1-7 na bei ikishuka huwa Debe ni Tsh 10 000-25 000 .Hii mara nyingi hutokea miezi ya 7-12.
Changamoto Usipozingatia maelekezo ya wataalam au wakulima wazoefu unaweza ukapata hasara kubwa.
By Agronomist Peter
Kwa kutoa order ya mbegu bora ya pilipili mbuzi/Pilipili Uganda, piga simu kwa kampuni ya AYEGRO Group Ltd Tz, kwa simu no. +255623642293 au 0744529070 au 0717529597 au 0625506080

Leave a Reply