Kilimo kisichotumia udongo kizuri, soma mahojiano haya na mwanadada mwammy na wewe ujifunze.

WAAFRIKA hasa Watanzania wamezoea kufanya kilimo kinachotumia udongo hali inayosababisha wakulima kumiliki heka nyingi kwa ajili ya shughuli hizo.

Katika miaka ya karibuni kumekuja na namna nyingine ya kufanya kilimo na mkulima anaweza kulima pasipo kutumia udongo.

Inaweza likawa ni jambo la kushangaza kwa wengi ambao hawajashuhudia kilimo hicho lakini ule usemi unaosema hakuna linaloshindikana chini ya jua unajidhihirisha hapo.

Kilimo cha bila kutumia udongo kimeingia nchini Tanzania na Mwamvua Mlanga maarufu kwa jina la Mwammy anakuwa ni balozi mzuri wa kilimo hiki.

Wiki hii JIONGEZE lilifanikiwa kufika shambani kwa Mwammy katika eneo la Afrikana, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambako ni heka moja tu lakini linamuingizia kipato kikubwa zaidi ya anayelima heka zaidi ya moja.

“Kilimo hiki ni kizuri kwa sababu ninavuna kila siku, kinafanyika kisasa pasipo kusumbua ardhi na maji yanayotumika ni kiasi kidogo,” anasema.

Anasema yeye analima mboga aina ya ‘lettuce’ inayotumika katika saladi na alianza kufanya kilimo hicho rasmi Oktoba, mwaka mwaka jana lakini kuvuna na kuuza alianza Aprili, mwaka huu.

Akizungumzia safari yake ya kuanza kilimo hicho, anasema alipata wazo la kuanza kulima baada ya kuamua kuacha kazi ya kuajiriwa lakini hakutaka kufanya kilimo kilichozoeleka. “Nimefanya kazi katika kampuni tofauti, nimefanya kazi katika Kampuni ya Vodacom kwa muda wa miaka 15 na kisha katika Benki ya NMB kwa muda takribani miaka miwili hata hivyo nilikuwa na hamu ya kujiajiri.

“Awali sikujua ninaweza kujiajiri kwenye nini lakini katika kutembeatembea nikapata wazo la kulima lakini sikutaka kufanya kilimo tulichozoea kukifanya enzi za wazazi wetu miaka hiyo ya nyuma, nilitaka kufanya kilimo cha kisasa,” anasema.

Anasema ndipo akajiingiza katika masomo nchini Israel na alijifunza kilimo cha bila kutumia udongo

bacho kitaalaam kinaitwa ‘hydronic.’ Anaelezea katika kilimo hicho nachotakiwa ni kujenga Green ouse kwa ukubwa wa eneo lako ukubwa unaotaka mwenye kisha afunga mabomba ya plastic yanayumika kama kitalu cha kupanda na kuzia mboga. “Kuna hatua ya kwanza tunaanza panda mbegu kila baada ya siku tu au wiki moja na zinakaa kwa siku , tunazimwagilia maji na tunatumia akumbi ya nazi yaliyosagwa na wekwa mbolea kama udongo kwa li ya kupandia. “Katika hatua hii tunawasha taa a ajili ya mmea kukua wakati wote a mchana na usiku pia kwa kuwa mea unakuwa kwa kutegemea wanga, ukizima taa ina maana usiku zo zinalala hivyo hazikui,” anasema. Kutokana na mazingira ya joto ni Dar es Salaam, anasema anaweka ni hivyo kuhakikisha hazipati ngasi na magonjwa mengine “Katika hatua hii ya mwanzo, semu ambayo mboga inatibiwa kwa wekwa dawa za magonjwa yote kaa hizo siku 15 (mara mbili au tatu) itoka hapo haziwekwi dawa yoyete vyo zinakuwa ni salama kwa kuliwa. aada ya stage hiyo zinapelekwa kaa stage ya primary ambayo ni meza nye matundu madogo madogo po mboga zinakuwa bado ndogo bazo zinakaa kwa muda wa siku zikitoka hapo zinakuwa zimekua vyo zinapelekwa kwenye stage ya kondari ambayo inakaa kwa siku 10 di 15 inategemea na hali ya hewa kwa wakati wa joto inaweza kupanda kutoka siku 35 hadi 40 baada hap tayari kwa kuvuna,” anasema.

Pia anasema mboga ikienda sokoni inakwenda ikiwa safi inakuwa haina udongo kwa kuwa inakuwa kwa kutumia mbolea na maji tu yanayopita kila baada ya dakika tano na inakuwa na mizizi yake unayoweza kuiweka kwenye maji na inaweza kukaa kwa siku saba.“Kila siku tunaangalia maji kama yamepungua na kuongeza ili mboga zisije kukosa maji,” anasema.

Anasema udongo unatumika wakati wa kupanda ambao hata hivyo si udongo wa kawaida bali ni makumbi ya nazi yaliyosagwa na kuwekwa mbolea baada ya pale unaweka kwenye mabomba yanayopitisha maji ambayo yanakuwa na mbolea ambazo ndizo virutubisho vinavyofanya mboga hizi zikue.

Anasema mbolea zinazotumika ni za kawaida tu kama zinazotumika katika mboga nyingine.

Anasema kwa sasa masoko yake ni katika supamaketi, hoteli za kitalii na migahawa. Anasema kwa siku anauza bachi 300 hadi 350 ambazo hutoka kila siku. Anasema katika kilimo hicho unaweza kulima strawberi, chinese, giligilani na mazao mengine jamii ya mbogamboga na matunda.

Akizungumzia changamoto anazokumbana nazo ni kupata vitendea kazi ambavyo ni mabomba yanayotumika kama shamba.

“Vitendea kazi ni gharama sana hivyo tunaomba Serikali hasa hii ya awamu ya tano yenye kauli mbiu ya uchumi wa viwanda kututengeneza pembejeo hizo kwa sababu ni sawa na matrekta katika kilimo cha kawaida.

“Wenzetu wanapunguziwa tozo mbalimbali katika pembejeo lakini sisi tunavyokwenda kununua viwandani hawajui kama tunakuja kulimia wao wanadhani tunakwenda kutumia katika ujenzi,” anasema.

Anasema changamoto nyingine ni green house (zinatengenezwa kwa chandarua na vyuma) kuuzwa kwa bei kubwa.

Pia anasema changamoto nyingine ni joto ambalo kwa Dar es Salaam linakuwapo kwa kipindi kirefu na inamfanya kutumia feni na kiyoyozi kupata hali ya ubaridi.

Pia anasema kwa kiwango kikubwa wanatumia umeme kuanzia kusukuma maji na hadi kudhibiti hali ya hewa.

“Tunategemea umeme katika shughuli zetu kwa asilimia nyingi lakini kama unavyojua umeme wetu si wa uhakika hivyo inabidi tuingie gharama ya kuweka majenereta,” alisema.

Anaeleza kuwa jambo jingine ambalo ni changamoto na anajitahidi kulidhibiti ni usafi na umakini.

“Kilimo hichi kinahitaji umakini wa hali ya juu, akiingia mdudu anaathiri mboga zote hivyo huwa nakuwa makini na nazuia watu kuingia.

“Ilishawahi kunitokea Agosti, mwaka huu kuna watu waliingia mboga zikaathirika na nikajikuta nachoma mboga zote hali iliyonifanya nishindwe kutoka nje kwa takribani wiki mbili lakini baada ya hapo niliinuka na kuendelea na kazi sikukata tama,” anasema.

Pamoja na kuanzisha kilimo hicho, anasema bado Watanzania hawajawa na mwamko na ufahamu wa kula mboga mbichi ambazo hazijapikwa.

Anasema katika kilimo hicho mkulima anaweza kuweka kumbukumbu vizuri na akajua faida na hasara mapema.

Anawashauri vijana na wakulima kupenda kujifunza na kufanya kilimo cha kisasa kwa sababu mradi unatumia eneo dogo na wafanyakazi wachache ukilinganisha na kilimo cha kawaida.

“Watu wengi wamekuwa na dhana kuwa kilimo ni kwa watu waliochoka hawezi kufanya kazi, mimi niliona ni vyema kuanza nikiwa kijana niliacha ajira nikaanza.

“Hivyo Watanzania wasiogope kuingia katika kilimo, katika kilimo hicho unaweza kulima chochote kwa sababu wanadamu ni lazima wale, fursa za kilimo zipo shambani, unaweza kupata zaidi kuliko anayeshinda ofisini,” anasema.

sikujua ninaweza kujiajiri kwenye nini lakini katika kutembeatembea nikapata wazo la kulima lakini sikutaka kufanya kilimo tulichozoea kukifanya enzi za wazazi wetu miaka hiyo ya nyuma, nilitaka kufanya kilimo cha kisasa,

source:www.pressreader.com/tanzania

Leave a Reply