KWANINI WENGI WANAPATA HASARA KATIKA KILIMO ?

KWANINI WENGI WANAPATA HASARA KATIKA KILIMO ?

Hasara katika kilimo zimekuwa ni jambo kubwa ambalo linasumbua vichwa vya wakulima wengi ndani na nje ya tanzania.Hasara katika kilimo huweza kusababishwa na mambo mengi sana lakini leo tutajifunza mambo machache.

1.Usimamizi mbaya.
katika mambo ambayo mkulima au mtu anayejihusisha na kilimo anatakiwa kuwa makini nacho ni usimamizi wa mazao au mifugo anayotaka au anayoifuga.Katika miaka ya karibuni kumeibuka na
wimbi la watu kujiingiza katika kilimo cha mazao au ufugaji kwa namna ambayo imewafanya wajutie kulima au kufuga,hii inatokana na wengi wao kwa namna moja au nyingine kula hasara za hali ya juu na wengine kupoteza makazi,mashamba au mali ambazo walikuwa wanazimiliki kwa sababu ya mikopo waliyoichukua.
Wengi ya wakulima hasa wale wanaojiingiza katika kilimo huku wakiwa na muda mchache sana wa kuangalia miradi walioianzisha na hivyo kuishia kufanya kile kinaitwa kilimo cha whatssap.Hii imewagharimu wengi na wengi wameishia kulia na kulaani kilimo kuwa si kitu/biashara ya kufanya.Lakini tatizo kubwa ni usimamizi mbovu wa miradi.

Ushauri.
Usianze kilimo kama huna uhakika na usimamizi wako au uangalizi wa mradi wako wa kilimo.

2.Kutokuwa na taarifa za uhakika.
Katika kilimo taarifa ni kitu mhimu sana kwa maendeleo na ufaulu wa mradi wako unaotaka kuufanya.Taarifa zinazo hitajika ni pamoja na:-
Eneo sahihi kwa mradi wako mf.zao kwa eneo sahihi.
Namna ya kuendesha mradi wako mf.unazalishaje mazao au mifugo.
Changamoto za mradi wako.
Soko na usafirishaji.n.k.
Ushauri.
Nini ,uzalishaje,wapi,lini,na kwanini.

3.Hali ya hewa.
Hali ya hewa ni mara nyingi si rahisi kuweza kuidhibiti,lakini unaweza ukapunguza uwezekano wa wa kupunguza hasara.

4.kilimo cha mali kuoza kwa kutumia kuvuli cha bei .
HIli pia limewaghalimu wengi kwa kulima kwa mihemko bidhaa ambazo huweza kuoza haraka kama nyanya kwakuvutiwa na bei ya mwaka jana. Mfano wengi sana wamekuwa wakiambiwa bidhaa hii au zao au mifugo hii inalipa basi wote wanaanza kuzalisha hiyo bidhaa na wengi wamejikuta wanaangukia kwenye bei mbaya au hata kufikia kiwango cha kutelekeza bidhaa hiyo sokoni.wengi kwa kulima kwa sababu ya mihemko wameingia kwenye madeni makubwa na benki au taasisis za fedha na hivyo kupoteza nyumba zao.
Ushauri.
usichukue mkopo bila kuwa na uhakika na kile unachokifanya na pia usingalie soko la bidhaa la zamani kuzalisha sasa.

Yapo mambo mengi ambayo ningekushauri kuhusu nanma ya kulima.
Insha Allah tukijariwa tutaendelea kujifunza zaidi🙏🏿🙏🏿

🌱🌱🌱🌱🌱🌱🌱🌱

Leave a Reply