MAGONJWA NA WADUDU KWENYE MATIKITI MAJI

Na

Ndg,dagras mwamlima.Mwanafunzi chuo kikuu cha kilimo sokoine (SUA) BSc.Agricultural economics and agribusiness (BSc.AEA)

MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU

Watakoaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea, ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kjupata dawa sahii.

Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu za majani na maua, na wengine hushambulia matunda, pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea.

Magonjwa kama ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe kabla hayajaleta madhara kwenye mimea. Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza kutumiwa kuthibiti magonjwa hayo hapo juu.

Vilevile matikiti hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na matunda. Dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda.

MAGONJWA YA TIKITI

1) UBWIRU CHINI (DOWNY MILDEW)

Huu ungonjwa husababishwa na fangasi (Pseudoperonosporacubensis).Ni kati ya mangonjwa yanayoshambulia majani na hupendelea sana wakati wa baridi,

 Dalili zake: Majani yaliyoshambuliwa hugeuka rangi na kuwa kama ya njano huku baadhi ya majani yakiwa kama yanakauka  na madoadoa meus kwa mbali..

Tiba yake.

Tafuta dawa yenye viambato…Metalaxyl na mancozeb ….kama vile Ridomil gold.

2) UBWIRU JUU (POWDERY MILDEW )

Dalili za huu ungonjwa…utaona majani yanakuwa kama yamemwagiwa unga ua majivu

Tiba yake

Tafuta dawa yenye kiambato…Difenoconazole ..kama vile Score.

3) KATA KIUNO.(DAMPING OFF)

Huu ugonjwa husumbua sana miche midogo,huanzia aridhini ,husababisha miche midogo kuanguka chini baada ya kula sehemu ya shina.

Tiba yake.

Tafuta Ridomil gold na anza kupulizia mara tu baada ya mimea yako kuota.

WADUDU

1) Wadudu mafuta (Aphid)

Hawa hushambulia majani na kufyonza juis ya mmea na baada ya kushambulia majani hujikunja na baadaye kupelekea mangonjwa ya virusi.

Dawa yao.

Tafuta Actara na pulizia majani pamoja na udongo. Wadudu wengine ni;Nzi weupe (whitefly )-Actara itawamaliza.,Utitiri mwekundu (Redspidermites)-Dynamec itawamaliza,Thrips-Actara na Dynamec itawamaliza kabisa.

UVUNAJI

Tikitimaji uvunwa baada ya miezi miwili na nusu hadi mitatu kutoka siku ya kupanda,lakin yapo ambayo hukomaa kwa siku 60-75 kutokana na aina ya mbegu. Ili kujua matikiti yamekomaa inahitaji ujuzi kidogo, upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano, pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu, ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake kama tunavyofanya kwenye mafenesi, hii nayo ni shule nyingine. Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi.

SOKO LA TIKITI

Napenda kuwashauri wakulima wetu kuwa njia nzuri ya kulima tikitimaji ni ile ya umwagiliaji, ukiwa mkulima wa tikitimaji lazima uwe mjanja kupanda zao lako ili uje uvune wakati soko liliwa vizuri, mzunguko mzuri wa kupanda tikiti ni huu, panda zao lako katikati ya msimu wa mvua wakati walimaji wa matikiti kwa kutegemea mvua (ambao ni wengi) mazao yao yametoa maua ili wakati wao wanavuna tikiti zao, mazao yako yawe ndio yanaanza kutoa maua kwa hiyo wakati unavuna wakulima wa kutemea mvua watakuwa washamaliza soko lao.Pia kwa wale wanaotegemea mvua ni vizuri uchunguze soko lako vizuri ili uwe na uhakika wa kuuza matunda yako wakati yakiwa tayari yamekomaa.  .acknowledged anzisha project Kwa mchango wao kuweza kuikamilisha hii makala fupi yenye faida kubwa sana Kwa  Mkulima.

Karibu agribusiness skills tujifunze njia za kilimo bora,kuongeza thaman ya mazao,ushauri kumbuka kilimo ni sayansi hivyo tufanye kilimo chenye Tija Na kibiashara ili tuongeze pato LA kaya Na taifa Kwa ujumla

Karibu sana

#nenda playstore pakua kilimosmartapp au bofya HAPA

Kwa makala nyingine kama hii tembelea page yetu ya agribusiness…. Kilimosmartapp Facebook Na instagram

Leave a Reply