Mbegu bora za mahindi MERU HB 513 (Ngamia)

MERU HB 515 Ni mbegu bora ya mahindi inayozalishwa na kampuni ya MERU AGRO TOURS & CONSULTANCY yenye makao makuu Arusha- Tanzania

SIFA ZAKE

 • Mbegu inayotumia mbolea kidogo nakutoa mavuno mengi (Nitrogen use efficient variety)
 • Inavumilia sana ukame
 • Ni mbegu kinzani/ stahimili na magonjwa ya majani (Baka kahawia, milia na kutu)
 • Mahindi yake yanafunga vizuri
 • Inazaa sana gunia (30-40) kwa Ekari moja
 • Inakomaa kwa muda wa siku 75-90 kwa ukanda wa kati na siku 100-110 kwa maeneo mengine
 • Ni mbegu yenye punje ngumu
 • Inazaa mahindi mawili mawili
 • Inastawi zaidi katika ukanda wa kati hadi wa juu (mita 1000-1800)

FAIDA KWA MKULIMA

 • Inakupa uhakika wa mavuno katika maeneo yenye mvua kidogo
 • Uhakika wa mavuno kwenye miaka ambayo mvua zinakatika mapema
 • Inakupa uhakika wa mavuno kwenye maeneo yenye magonjwa ya majani
 • Mahindi yake hayawezi kupata magonjwa ya gunzi muozo (cob rot)
 • Itakuhakikishia mavuno mengi na faida kubwa katika shamba dogo
 • Inafaa sana kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa hasa nyanda za juu
 • Inakoboreka vizuri na kutoa unga mwingi
 • Mahindi yake ni matamu kwa kuchoma
 • Inasitawi maeneo mengi hapa nchini.

kwa mawasiliano katika mikoa yote piga +255753 993 481

Leave a Reply