Mbegu bora za mahindi MERU HB 623 (Kiboko)

MERU HB 623 Ni mbegu bora ya mahindi inayozalishwa na kampuni ya MERU AGRO TOURS & CONSULTANCY yenye makao makuu Arusha- Tanzania

SIFA ZAKE

 • Inavumilia sana ukame
 • Ni mbegu kinzani/ stahimili na magonjwa ya majani (Baka kahawia, milia na kutu)
 • Mahindi yake yanafunga vizuri
 • Inazaa sana gunia (40-50) kwa Ekari moja
 • Inakomaa kwa muda wa siku 120-140
 • Ni mbegu yenye punje ngumu
 • Inazaa mahindi mawili mawili
 • Inastawi zaidi katika ukanda wa kati hadi wa juu

FAIDA KWA MKULIMA

 • Inakupa uhakika wa mavuno katika maeneo yenye mvua kidogo
 • Uhakika wa mavuno kwenye miaka ambayo mvua zinakatika mapema
 • Inakupa uhakika wa mavuno kwenye maeneo yenye magonjwa ya majani
 • Mahindi yake hayawezi kupata magonjwa ya gunzi muozo (cob rot)
 • Itakuhakikishia mavuno mengi na faida kubwa katika shamba dogo
 • Inafaa sana kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa hasa nyanda za juu
 • Inakoboreka vizuri na kutoa unga mwingi
 • Mahindi yake ni matamu kwa kuchoma
 • Inasitawi maeneo mengi hapa nchini.

kwa mawasiliano katika mikoa yote piga +255753 993 481

2 comments on “Mbegu bora za mahindi MERU HB 623 (Kiboko)

 1. Asanteni Ila muifikie jamii zaidi kwa maana kwa sasa mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri Sana upatikanaji wa mvua ya kutosha ambayo awali iliwasaidia kwa kuletwa kwa mbegu hiyo ni mkombozi kwao

Leave a Reply