Mbegu bora za nyanya pamoja na sifa zake.

Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine duniani.

Zao la nyanya linalimwa karibu maeneo yote ya Tanzania. Uzalishaji wa nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga yanayolimwa hapa Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni jumla ya tani 129,578 ikiwakilisha asalimia 51 ya mazao yote ya mboga

Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo ya Tanzania, maeneo yanalolima sana nyanya ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida. Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 (ekari 15,398). Pamoja na kwamba eneo la uzalishaji linaongezeka kwenye maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana.

Uzalishaji mdogo unasababishwa na kupungua kwa rutuba ya ardhi, upepo, joto, ukame. Sababu nyingine ni pamoja na ukosefu wa aina za nyanya zenye mavuno mengi amabazo zinahimili mazingira ya kwetu, wadudu, magonjwa na magugu.

MBEGU BORA ZA NYANYA

1. EDEN F1

         SIFA ZA EDEN F1

 • Hukomaa mapema; baada ya siku 70
 • Mmea wenye afya na majani yakutosha
 • Yenye matunda mengi ya gredi 1, yenye ganda ngumu inayoyafanya yawe rahisi kuisafirisha
 • Matunda yake inadumu kwa muda wa siku kumi na nane
 • Inahimili maradhi ya mwozo aina ya Alternaria stem Canker, mnyauko aina  ya Verticilium,  Mnyauko aina ya   Fusarium Wilt, Minyoo fundo (Nematodes), Gray leaf Spot na Bacterial Speck
 • Mavuno yake ni kati ya tani 45 – 50 kwa ekari
 • Mazao kwa kila ekari Tani 45-50 ama matenga 750-833

2. ASSILA F1

hii ni mbegu chotara ambayo ni stahimilivu sana kipindi cha kiangazi(ukame)  yenye sifa zifuatazo

Kiwango cha mavuno ni kreti 417 za kilo 60 kila moja sawa na Tani 25 kwa ekari moja

SIFA  ZA ASSILA F1

 • Ni aina fupi ya nyanya yenye mazao bora ya soko na ubora wa kusindika
 • Duara butu lenye rangi nyekundu ya kupendeza
 • Gredi 1-3 tunda la kiasi la uzani wa gram 90-120 na lenye kudumu
 • Ni tamu na hupatia chakula ladha nzuri
 • Mmea unakomaa haraka tunda stahimili kwa magonjwa
 • Hukomaa kwa mda wa siku 75 (miezi 2 na nusu)
 • Ina kinga ya mapema dhidi ya maradhi ya virusi vya nyanya

3. ANNA F1:

hii ni mbegu chotara ambayo ni maalum kwa kilimo cha ndani yaani  GREENHOUSE

Kiwango cha mavuno ni Tani 74 kwa Ekari (80-90kg/m2)

SIFA ZA ANNA F1

 • Inasitawi vizuri ziadi kwenye greenhouse pia inafanya vizuri sehemu ambazo hazina green house
 • Matunda yake ni ya mviringo na mekundu
 • Ni mbegu kizani kwa magonjwa ya nyanya kama vile (Alternaria stem canker, Verticillium,Fusarium wilt na  nematodes)
 • Inakomaa ndani ya siku 75 baada ya kuhamisha kweye kitalu.

IJAYO: MAGONJWA YANAYOSUMBUA NYANYA NA MATIBABU YAKE.

Imeandaliwa na:  Edward Costantine

Email:  costeredward1@gmail.com

 

1 comment on “Mbegu bora za nyanya pamoja na sifa zake.

Leave a Reply