UANDAAJI WA BWAWA LA KUFUGIA SAMAKI

MBINU BORA ZA UFUGAJI WA SAMAKI – SOMO LA PILI

Bwawa la kufugia Samaki; Hii ni nyumba ya Samaki. Kama wewe unavyo hitaji makazi bora, pia afya ya Samaki wako inategemea sana ubora wa bwawa unalo wafugia pamoja na ubora wa maji bwawani. Katika somo la Mbinu bora za ufugaji wa Samaki lililopita nilielezea mazingira sahihi ya kuchimba bwawa la kufugia Samaki ambayo yanafaa kuchimba bwawa la kawaida lisilohitaji kujengewa wala kufanyia maboresho zaidi. Katika somo hili nitafundisha namna ya kuandaa mabwawa aina tofauti.

Ukubwa wa bwawa; Ukubwa wa bwawa hutegemea eneo ulilo nalo na idadi ya samaki unaohitaji kufuga. Kwa kawaida eneo la mita moja ya mraba hukaa samaki watano. Hata hivyo unaweza kuongeza idadi ya Samki hadi kufikia Samaki 30 kwa kila mita moja ya mraba iwapo utaweka mifumo ya kuongeza hewa bwawani na kuhakikisha usafi wa maji wa hari ya juu.

Mfano

Kwa hawaida bila kuweka mifumo ya kuongeza hewa nay a kusafisha maji, kama ukiwa na bwawa lenye urefu wa mita 100 na upana wa mita 50 litakuwa na ukubwa wa jumla ya mita 5,000 za mraba.

100m × 50m = 5,000m

5,000 × 5 = 25,000

Kwa maana hiyo basi katika eneo mita 5,000 za mraba utafuga jumla ya samaki 25,000.

Kina cha bwawa; kwa kawaida bwawa la kufugia Samaki huwa na kina cha mita moja na nusu (1.5m), isipokuwa bwawa la kufugia Sangara lenyewe huwa na kina cha mita 2.5 kwasabau Sangara ni wakubwa na wanahitaji maji mengi pamoja na nafasi kubwa ya kuishi. Wao huwekwa watatu kwatika mitamoja ya mraba na kama unahitaji kuwafuga wawe wakubwa sana hadi kufikia kilo 200 na kwendelea unaweka mmoja kwa kila mita moja ya mraba.

AINA / MADARAJA YA MABWAWA

Mabwawa yamegawanyika katika madaraja makuu matano;

 1. BWAWA DARAJA LA KWANZA

Hili ni bwawa la kawaida ambalo huchimbwa ardhini na kisha kujazwa maji, tayari kwa ufugaji. Uingizaji wa maji katika bwawa hili hutegemea chanzo kikubwa cha maji kilichopo karibu na bwawa, hususani mto au chemchemi kubwa. Bwawa hili ni lazima liwe katika eneo lenye udogo unao twama maji.

 1. Uchimbaji wa bwawa daraja la kwanza; Anza kuchimba bwawa kwa kutumia mikono au Katapira (Trector). Chimba kwa ukubwa unaoweza / unao hitaji. Liwe na kina chenye urefu wa mita moja na nusu.

 2. Maandalizi ya bwawa; kwa ajili ya usalama wa mbawa na Samaki wako, maandalizi ya bwawa yazingatie hatua muhimu zifuatazo;

 1. Chimba mtaro wa kuingiza maji bwawani na kutengeneza njia ya kutolea maji bwawani.

 2. Chimba shimo karibu na bwawa ambalo maji yataingia ili kuacha matope, maji yaingie bwawani yakiwa hayana tope. Kutoka humo shimoni yaingie bwawani kupitia bomba au mfereji safi. Shimo hilo utakuwa unalisafisha mara kwa mara kuondoa tope. Vinginevyo bwawa lako litachafuka na litakuwa linapungua kina kila siku na utapata gharama kubwa kulichimba tena kuondo tope.

 3. Weka chujio unapoingizia maji na unako yatolea ili kuzuia Samaki wasitoke bwawani na Samaki wa mtoni wasiingine bwawani.

 4. Usiruhusu maji kuingia ovyo bwawani.

 5. Tengeneza sehemu ya kulishia Samani ambayo atakayekuwa anawalisha Samaki kila siku atakuwa anasimama. Ni muhimu ikawa na ngazi za kushukia.

 6. Weka kichanja cha fito kwenye kona moja ya bwawa ambacho mlishaji atasimama wakati anawapa Samaki chakula.

 7. Sambaza chokaa kwenye bwawa lako, iache kwa muda wa wiki moja bila kuingiza maji. Chokaa husaidia kuuwa wadudu na vimelea vya magonjwa.

 8. Baada ya wiki moja, weka kinyesi cha ngombe kibichi kwenye bwawa lako. Kinyesi hicho kifungwe kwenye mfuko wa kiroba na kisha kuweka bwawani. Weka viroba viwili gadi 8 kilingana na ukubwa wa bwawa lako. Baada ya kuweka kinyesi, ingiza maji bwawani kwa ujazo wa mita moja, nusu ibaki bila maji. Yaache yakae kwa muda wa siku tano ili kinyesi kioze na kubadirisha rangi ya maji bwawani kuwa ya kijani. Fanya zoezi la kukamua viroba nyenye kinyesi cha ng’ombe kila siku asubuhi na jioni kwa muwa wa siku tao kisha vitoe bwawani. Bwawa liko tayari kwa kuingiza vifaranga.

Zingatia; kinyesi cha ng’ombe kwenye bwawa la samaki husaidia kutengeneza chakula cha samaki cha asili kwenye bwawa, na kupunguza uangavu kwenye maji kwa ajili ya afya ya Samaki.

Mfano wa bwawa daraja la kwanza

Pata ushauri wa wataalam; Ushauri wa wataalamu ni muhimu kwa kila hatua. Usifanye jambo

lolote kwa kubahatisha, mshirikishe mtaalamu katika hatua zote kwa mafanikio zaidi ya mradi wako.

  1. BWAWA DARAJA LA PILI

Hili ni bwawa zuri la kufugia kwa malengo. Uchimbaji na uandaaji wake hufanana na wa bwawa la daraja la kwanza isipokuwa lina tofauti zifuatazo:

 1. Baada ya kuchimbwa hujengewa ukuta imara kwa kutumia Tofari / Slabs na vifaa vingine.

 2. Huweka zege chini na sakafu ili kuzuia upotevu wa maji.

 3. Linafaa kufugia hata katika sehemu zenye uhaba wa maji.

 4. Uhudumiaji wa Samaki ni rahisi na ni rahisi kulifanyia usafi.

 5. Ni rahisi kuliwekea mifumo ya kuongezea hewa na kusafisha maji ili yatumike kwa muda mrefu bila kubadirishwa.

 6. Ni rahisi kudhibiti vimelea vya magojwa katika bwawa hili.

 7. Ni rahisi kudhibiti ongezeko la samaki kupita kiasi.

 8. Ni rahisi kutumia maji ya bomba au chanzo kingine.

   

Ujenzi wa bwawa daraja la pili:

 • Vifaa kama kokoto, Simenti, Mchanga, Nondo na vingine hutumika katika ujenzi wa bwawa hili.

 • Lisizidi ukubwa wa mita za mraba 400 maana maji yana nguvu sana na yakiwa mengi zaidi yanaweza kulivunja/ kulipasua.

 • Kuta zake ziwe imara, ziimarishwe kwa nguzo ikiwezekana funga kwa nondo ili kuepuka kupasuka kwa ukuta ambako hupelekea hasara kubwa.

 • Weka mfumo wa kudumu wa kuingiza maji na chemba ya kutolea maji yenye chujio jembamba kwa ndani.

 • Unaweza kuweka Ligning (naironi ngumu) badala ya kujenga ukuta na sakafu.

 • Shirikisha mtaalamu katika hatua zote za maandalizi na ujenzi.

   1. BWAWA DARAJA LA TATU.

Liko sawa na bwawa daraja la pili lakini limezidi haya yafuatayo;

 • Ni la kisasa zaidi.

 • Lina mifumo ya kisasa ya kuongeza hewa, kusafisha maji na kulisha Samaki kwa wakati bila mtu kuhusika.

 • Mifumo yake hutumia umeme mdogo sana.

 • Unaweza kuweka mfumo mmoja au yote kulingana na mahitaji yako na uwezo wako.

 • Lina uwezo wa kubeba Samaki wengi yani 15 – 30 kwa kila mita moja ya mraba.

 • Ni rahisi kudhibiti ongezeko la samaki wanapozidi kiasi.

 • Uendeshaji wake ni rahisi na mavuno yake ni ya uhakika.

   1. BWAWA DARAJA LA NNE.

Ni Bwawa ka kuhamishika.

Lina sifa zote sawa na bwawa daraja la tatu lakini linazidi kwa sifa ya kuhamishika. Unaweza kulihamisha likiwa na maji pamoja na Samaki lakini pia kama unahamia mbali unaweza kulikunja na kuondoka nalo.

NaGA FISH FARMING SERVICES DEPARTMENT (NFFSD) tumeiendeleza Sana tekinolojia ya mabwawa haya ya kuhamishika pamoja na yenye mifumbo mbalimbali na kuipa jina la NaGA FISH TECHNOLOGY. Ni rahisi kutumia na ni rahisi kuyamudu.

   1. BWAWA DARAJA LA TANO.

Bwawa la juu.

Hili hujengwa juu ya nyumba au bwawa juu ya lingine. Kwa Tanzana ni NaGA FISH FARMING SERVICES DEPARTMENT (NFFSD) pekee tulio na tekinolojia hii.

 

source: https://nagamedia.co.tz/2018/04/09/uandaaji-wa-bwawa-la-kufugia-samaki/

Leave a Reply