Ufuatiliaji mazao kwa ajili ya wadudu na magonjwa

Ufuatiliaji mazao kwa ajili ya wadudu na magonjwa

Kwa wadudu na magonjwa mengi, tatizo likionekana mapema huwa bora zaidi: itakuwa rahisi kuchukua hatua ili kusaidia kuzuia hasara kubwa kutokea au kuzuia mdudu au ugonjwa kuenea kwa mazao yote na hata mbele kwa mashamba jirani.

Njia bora ya kufanikisha hili ni kukagua mazao mara kwa mara kwa kuzingatia utaratibu. Njia moja ya kufanya hivyo ni kutembea ndani ya shamba kufuatia muundo wa umbo M; hii itahakikisha kuwa mkulima haangalii pembezoni pekee bali pia katikati.

Kama matatizo yoyote yameonekana, mkulima lazima achunguze mimea kwa makini ili aone dalili za tatizo na fununu za visababishi vyake.

Dalili za mazao zinaweza kuwa pamoja na:

 • Je mmea umenyauka – yaani hauna nguvu za kusimama wima kama kawaida na umeinama?
 • Je, majani yana rangi ya manjano zaidi kuliko kawaida?
 • Je, majani yamebadilika rangi kutoka kijani na kuwa na rangi nyingine isiyokuwa manjano?
 • Je, mimea ni midogo kuliko ilivyo kawaida?
 • Kuna sehemu za mmea zilizokufa?
 • Kuna miundo ya milia isiyokuwa ya kawaida kwenye majani na mashina?
 • Je, majani yana madoa juu yake?
 • Je, majani yametafunwa – je, yana mashimo yanayoonekana kama yameliwa?
 • Je, kuna dalili ya wanyama ambao wamefanya hivi?
 • Je, majani yana malengelenge ama yamekunjikakunjika?
 • Je, majani au matunda yana umbo lisilokuwa la kawaida?
 • Je, majani ni madogo kuliko kawaida na/au yameshikana pamoja kuliko kawaida?
 • Je, majani yana michoro ya kijani chepesi na njano yakionekana kuwa na batobato?
 • Je, kuna alama za kahawia pembezoni mwa majani?
 • Je, kuna umbo lililomea lisilokuwa la kawaida juu ya majani au sehemu nyingine za mazao?
 • Kuna tundu kwenye mashina na nafaka?
 • Kuna vimbe juu ya majani au sehemu nyingine za mmea?
 • Je, sehemu za mmea zinaoza – yaani, zinakuwa laini na rojorojo?

Kama yoyote kati ya dalili hizi imeonekana, mkulima anahimizwa kutafuta usaidizi kutoka kwa mfanyakazi wa ugani, mkulima mwenye ujuzi aliye karibu naye au muuzaji bidhaa za kilimo au kituo cha utafiti kilicho karibu.

6 comments on “Ufuatiliaji mazao kwa ajili ya wadudu na magonjwa

Leave a Reply