UFUGAJI WA SAMAKI KISASA

KWA ENEO NA GHARAMA KIDOGO FUGA SAMAKI WENGI NA BILA KULAZIMIKA KUCHIMBA ARDHI

1.Tunaelimisha jamii kuhusu teknolojia mpya za ufugaji samaki kisasa

 

2.Tunawajengea wateja wetu mabwawa yakisasa ya ufugaji samaki yanayojengwa kutumia mabanzi au yale ya kuhamishika ambayo mara nyingi tunatumia chuma na turubali maalum

 

 

3.Tunawauzia wafugaji wa samaki kila wanachohitaji kufanikisha ufugaji wa samaki kisasa, ikiwemo vyakula, na mabwawa yaliyotayari na mbegu bora ya samaki kwa gharama nafuu.

 

4.Tunatoa huduma za ushauri wa kitaalam zaidi kwa wale wafugaji walioanza ufugaji samaki kisasa kwa kujengewa nasi kwa teknolojia tunazowajengea au kuwauzia.

 

 

5.Tunatoa ushauri wa kuhusiana na upatikanaji wa soko la samaki haswa kwa wafugaji walioanza kufuga kwa msaada wetu.

 

6.Malengo yetu nikufanya ufugaji samaki kuwa rahisi kadiri iwezekanavyo, utumie eneo dogo kwa uzalishaji mkubwa, hii tunafanya kwa kutumia ubunifu na kuchanganya teknolojia yetu na ya ufugaji samaki kwenye mataifa yaliyoendelea iwe rahisi kufanyika kwa mazingira yetu.

 

 

7.Tuna malengo yakuzalisha minofu ya samaki na na bidhaa nyingine zitokanazo na samaki kwa soko la ndani na la nje, hivyo mbeleni tutafanya ufugaji wa kimkataba na wafugaji  wa samaki waliokwishabobea kwenye ufugaji huu wa kisasa chini ya uangalizi wetu nakuwaakikishia soko la samaki watakaozalisha.

 

UFUGAJI SAMAKI

Kwa miaka mingi imekuwa kawaida kwa watu wanapotajiwa ufugaji wa samaki moja kwa moja hupata picha au kuanza kufikiria mchakato wakupata makatapila au mtaji mkubwa kuchimba mabwawa.

Positive eye Co. Ltd inakuwa kampuni  ya kwanza kabisa kutambulisha Tanzania ufugaji wa samaki kisasa  na kibiashara katika mabwawa yasiyochimbwa ardhini ambayo yamekuwa yakitumika katika nchi nyingine mbalimbali ikiwemo Kenya kwa kitambo sasa, na hata sasa kampuni hii imeweza kubuni  na inaendelea na tafiti zakibunifu za aina nyingine ya mabwawa  ambayo hufaa kuamishika kwa wafugaji wanaokaa eneo lisilokuwa lakudumu au nyumba yakupangishwa kunufaika na ufugaji samaki.

Katika teknolojia hii ya ufugaji samaki kisasa, tofauti na inavyofaamika kitaalamu na ilivyosomwa na wataalam wetu wa kilimo kwa miaka mingi kuwa utaweza kufuga samaki 3-4 tu kwa eneo la mita moja mraba. Kwenye ufugaji huu teknolojia na uwezo wakuthubutu kujiongeza kijasiriamali vimebadilisha mambo, kwani utahitaji eneo la mita 4 urefu, mita 2 upana na mita 1 kina kuwezakufuga samaki 1000 aina ya kambale au wastani wa tilapia 300-400 na kulazimika kubadili maji nusu ya ujazo mara moja tu kwa wiki.

Kutengenezewa mabwawa haya utahitaji kuwa na mirunda kidogo na mabanzi ambayo yatatumika kutengeneza umbo la bwawa la samaki kwa kuinua juu bila kulazimika kuchimba chini na baada ya hapo yatawekewa karatasi maaalum yakuhifadhi maji(tazama picha hapo chini kwa uelewa zaidi). Karatasi hizi ziko za aina tofauti zikitofautiana kwa ubora na muda wakudumu, Japo wengi huanza mradi huu kulingana na uwezo wakimtaji wa mhusika lakini sisi tunashauri aina bora ya karatasi ambayo ni gharama juu kidogo kuinunua lakini inawezakudumu kwa wastani wa miaka hadi 30 endapo itatunzwa vyema

Katika ufugaji huu wa samaki kisasa samaki aina ya kambale watawezakufikia kuvunwa yaani uzito wa kati ya 1-1.5kg ndani ya kipindi cha miezi 6-8 tu, kutegemeana na sababu mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa chakula bora ,hali joto ya wastani mzuri ambavyo huchangia ukuaji wa haraka wa samaki na maji.

TATHMINI YA UZALISHAJI, SOKO/UHITAJI WA SAMAKI DUNIANI

Imethibitika upatikanaji wa samaki kwenye vyanzo vya asili umekuwa ukiendelea kuporomoka kutokana na uvuvi haramu, uchafuzi wa maji na kemikali toka viwandani, n.k,huku uhitaji wa nyama nyeupe umekuwa ukiendelea kuongezeka kwa kasi siku hadi siku. Tathmini inaonyesha miaka ya 1970 ni wastani wa 5% tu ya samaki walioliwa duniani walitoka kufugwa, Hivi leo nusu ya kiwango cha samaki wanaoliwa duniani ni wakufugwa, na baadhi ya wanasayansi wametabiri hadi ifikapo mwaka 2048 hazina ya samaki wote wapatikanao kwenye vyanzo vya asili itakuwa imekwisha hivyo kulazimisha uhitaji wote wa samaki duniani kutoshelezwa kwa samaki wafugwao kibiashara mashambani mwetu, hivyo kuthibitisha fursa ya kuzalisha samaki kulisha dunia na idadi kubwa ya watu inayoongezeka kwa kasi kuliko uzalishaji wa chakula kinachohitajika mwanadamu kuishi vyema.

Tembelea: http://www.telegraph.co.uk/news/uknews/1533125/All-seafood-will-run-out-in-2050-say-scientists.html

Kanuni ya uhitaji na uzalishaji (demand & supply principle)

Kanuni ya kiuchumi ya uzalishaji na uhitaji inasema “mara zote kunapokuwa na uhitaji mkubwa wa bidhaa yeyote  sokoni kuliko kiwango cha uzalishaji au upatikanaji wake basi bei itakuwa juu” na vivyo hivyo uzalishaji ukiwa mkubwa kuliko uhitaji bei ya bidhaa hiyo itakuwa chini. Kwa kutumia kanuni hiyo fanya ufuatiliaji utagundua nyama ya samaki inauzwa ghali kiasi cha watu wengi wa kipato cha chini  na kati kutomudu kuitumia kadiri wapendavyo. Na hiyo ni ishara yakuwa soko lake lipo ni kubwa.

KWA UJUMLA BISHARA YAKUZALISHA CHAKULA NI BISHARA AMBAYO SOKO LAKE LIPO SIKU ZOTE AU KAMA NI LAKUTAFUATA AU KULITENGENEZA NI RAHISI SANA SABABU MWANADAMU KABLA YA MAMBO MENGINE YOTE KULA NI SUALA LA LAZIMA ILI AWEZE KUISHI.

 

Jumla kuu gharama yakuanza mradi kisasa  2,043,700

FAIDA (BAADA YAKUTOA GHARAMA ZAUENDESHAJI) 2,600,000

Tazama chart ya maelekezo hapa Positive eye co ltd

 

 

Leave a Reply