UGONJWA WA MAHEPE.

Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao hushambulia zaidi kuku, bata maji na bata mzinga. Kuku wa mayai
ndio wanaoathirika zaidi. Mara nyingi ugonjwa hutokea katika kuku wenye umri kati ya wiki 12 hadi 24, ijapokuwa
hata kuku wakubwa nao hupata ugonjwa.

🌀Huu ni ugonjwa unaowapata kuku, ambao unasababishwa na kirusi aina ya “HERPES VIRUS”.

Jinsi Ugonjwa Unavyoenea

• Maambukizi pia kuenea kupitia mfumo wa hewa, kwa vumbi lenye vimelea katika mabanda na vumbi
litokanalo na manyoya.

• Mate ya kuku wagonjwa pia ni njia mojawapo ya maambukizi

• Binadamu, inzi na aina nyingine za ndege pia zinaweza kusambaza maambukizi.

Dalili za Ugonjwa wa Mahepe (Mareck’s Disease)

Dalili

• Uharo mweupe wenye maji maji
• Mboni ya jicho kuwa na rangi ya kijivu
• Upofu kwenye kuku
• Miguu na mabawa hupooza
• Kuku kupindisha kichwa
• Kwa kawaida vifo ni kati ya asilimia 10 na 80.

Uchunguzi wa Mzoga

• Uvimbe mweupe karibu katika viungo vyote laini vya mwili: maini, figo, bandama na ngozi.
• Mishipa ya fahamu kuvimba katika miguu na mbawa zilizopooza

Kuzuia na Kinga

• Mizoga, makapi na vifaa vingine vilivyochafuliwa na kuku wagonjwa vichomwe moto au kuzikwa.
• Weka utaratibu madhubuti wa kupuliza dawa za viuatilifu vinavyofaa
• Baada ya kumaliza kuwauza kuku wote, fanya usafi wa mabanda na kupuliza dawa
• Hakikisha unatenganisha kuku wadogo na wakubwa hadi miezi 3, na watenganishe kuku kwa umri
• Vifaranga vya siku moja vipatiwe Chanjo dhidi ya ugonjwa

Tiba:✅
Hakuna matibabu yaliyogundulika kisayansi, ila kama ugonjwa huu umeingia katika mifugo yako tenganisha wazima na wagonjwa kuku wapatiwe chakula cha kutosha na vitamini muda wote.

Leave a Reply