UPANDAJI WA BAMIA.

UPANDAJI WA BAMIA

Mbegu za bamia mara nyingi husumbua kidogo kuota kama patakuwa na hali ya baridi katika udongo.Hivyo ili ziote vizuri tunashauriwa kabla ya kuzipanda shambani ziloweke katika maji ya uvuguvugu kwa masaa 24 au ziloweke kwa dakika 30 katika ethly alcohol and acetone,.
panda mbegu zako katika mashimo uliyoyachimba katika udongo wenye unyevu kwa kina cha sentimeta 2 -3 katika nafasi ya sentimeta 60-90 kati ya mstari na msatari na sentimeta 25-50 Kati ya shina na shina utahitajika katika kila shimo uweke mbolea kwa ajili ya ukuaji mzuri wa Bamia zako
kutumia mbolea ya kuku au ng’ombe amabayo ni bora zaidi kwani ya kuku huisha kazi yake mapema zaidi katika udongo.Panda Mbegu mbili kwa kila shimo na zikisha ota ngolea uache shina moja kwa kila shimo.kiasi cha kilo 1.5 – 2.5 hutosha kwa ekari moja ambapo wingi wa mbegu itategemea uwezo wa mbegu kuota na aina ya bamia.Kama mbegu zako uwezo wake wa kuota ni mdogo mbegu zitatumika nyingi na kama unapanda bamia fupi au bamia zenye mbegu kubwa mbegu itatumika nyingi pia.Mbegu za bamia zinaweza kuchukua siku 8 – 10 kupanda hadi kuota.Pia bamia unaweza kupanda mbegu katika kitalu baadaye zikifikisha sentimeta 10-15 unazing’oa na kwenda kupanda shambani ila njia nzuri ni kupanda moja kwa moja shambani

Leave a Reply