UTATUZI WA UAGIZAJI WA MAFUTA YA KULA NJE KWA KUWEKEZA KWENYE KILIMO CHA CHIKICHI.

Takwimu za chama cha wasindikaji wa mbegu za Alizeti(Tasupa),zinaonyesha mahitaji ya mafuta ya kula nchini ni Tani 570,000 kwa mwaka lakini uzalishaji wa ndani ni Tani 210,000 tu ambapo Tani 180,000 zinatokana na Alizeti wakati vyanzo vingine vikichangia Tani 30,000 hivo zilizobaki Tani 260,000 Taifa hulazimika kuagiza kutoka nje na takwimu za Benki kuu ya Tanzania(BoT) zinaonyesha zaidi ya Sh600 bilioni hutumika kila mwaka kuagiza nakisi ya mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.

Tanzania huzalisha Tani 100,000 za Alizeti kwa mwaka ambazo hutoa Tani 25,000 za mafuta za mafuta zikikamuliwa na wakulima pia wakulima wa pamba katika kanda ya ziwa wanavuna Tani 80,000 wanachangia Tani 10,000 za mafuta baada ya mbegu za pamba kukamuliwa.

Kiasi kikubwa cha mafuta ya kula kinachozalishwa nchini kinatokana na Alizeti lakini wadau wa sekta hiyo wanaamini uwekezaji wa kina ukifanywa kwenye chikichi/mawese upungufu uliopo utabaki historia .Kilimo cha chikichi kinamuwezesha mkulima kuvuna mara3-4 kila mwaka baada ya kupanda hivyo uwekezaji ukifanyika kwenye kilimo hiki Tanzania haitaagiza mafuta ya kula kutoka nje tena.

Kigoma ndio mkoa maarufu zaidi kwa kilimo hiki ikiwa na historia ya kulima chikichi na kukamua mawese tangu 1920 .Kwa sasa maeneo mengine yanayolima zao hilo licha ya kigoma ni Kyela ,baadhi ya maeneo ya Tanga na Nyasa.

Leave a Reply