ZINGATIA YAFUATAYO KABLA HUJALIMA.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUFANYA KILIMO.

  1. AINA YA KILIMO MKULIMA ANACHOTAKA KULIMA.

Kuna aina tatu za  kilimo ambacho kabla ya mkulima kufanya kilimo anatakiwa kujua anafanya kilimo cha aina ipi na kwa sababu ipi.Aina za kilimo ni:

  • Kilimo cha mvua

-Hiki ni kilimo ambacho hutegemea msimu wa mvua katika kukifanya na kufanikiwa .Kilimo hiki sio kizuri kwa kilimo biashara maana majira ya mvua yakibadilika tu na mkulima anaweza pata hasara sana lakini kilimo hiki kinafaa kwa wanaolima kwa ajili ya kulisha familia zao na mifugo yao tu.

  • Kilimo cha kumwagilia

-Hiki ni kilimo kisichotegemea mvua na ni kilimo kizuri sana kwa kilimo biashara kwani kinampa mkulima uhakika wa kuvuna mazao mengi Zaidi Zaidi mkulima anapaswa kujua ni wakati upi anapaswa kumwagilia na miundombinu gani aitumie katika kufanya umwagiliaji wake.

 

  • Kilimo cha bandia

-Hiki ni kilimo cha kisasa ambacho kinahitaji miundombinu mizuri na ya kisasa Zaidi.Kilimo hichi pia ni kilimo kizuri kwa kilimo biashara lakini mkulima anapaswa kuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na kilimo hichi.Kilimo hichi hufanyika mahali popote iwe mjini au kijijini pia katika eneo dogo na eneo kubwa kilimo hiki kinafanyika.Hapa panahusisha greenhouse na hydroponic (kilimo cha kwenye mabomba bila udongo au kwa udongo).

  1. MUDA WA KUFANYA KILIMO.

Mkulima anapaswa kuzingatia muda sana   na kujua zao husika linapaswa kulimwa wakati gani,kupaliliwawakati gani,kuvunwa wakati gani,kuhifadhiwa wakati gani na kuuzwa wakati gani.Lakini muda unaendana na aina ya kilimo ambayo mkulima anatarajia kulima yaani mfano mkulima analima kilimo cha mvua hivyo anapaswa kujua wakati gani anapaswa kulima kwa kuzingatia majira ya mvua bila kuchelewa.Pia mkulima anaefanya kilimo cha aina yoyote pia anatakiwa kuzingatia muda wakati wa kufanya kilimo ili kujua ni wakati gani aina ya zao hilo linahitajika sokoni hasa kama mkulima anafanya kilimo biashara.Na kwa ufupi muda ndio mtaji wa kwanza katika kilimo kabla ya fedha na vifaa maana mkulima anapaswa kulima kwa wakati,kupanda kwa wakati,kuweka mbolea kwa wakati,kupalizi kwa wakati na kuvuna kwa wakati.

 

MASOKO YA MAZAO NA MIFUGO.

Ukweli ni kwamba soko ndio msingi mkubwa pia katika kilimo na ufugaji.Mkulima akikosa soko ni wazi atakuwa amewekeza pesa zake bure katika kilimo/ufugaji na wakati mwingine hupelekea mazao kuozea shambani hivyo mkulima kabla ya kulima anapaswa kuhakikisha ana soko la kutosha kabisa kabla ya kuingia katika kilimo/ufugaji.

Vilevile kabla ya kufanya kilimo pia mkulima anapaswa kujua soko lake ni lipi yani atauza shamba,atauza kupitia dalali au atapeleka kwa watumiajai moja kwa moja ,yote haya mkulima anapaswa kuyafahamu kabla ya kuingia rasmi katika kilimo au ufugaji kusudi pesa zinazowekezwa na mkulima huyo katika kilimo/ufugaji zilete faida na kubadilisha maisha ya mkulima.

UHIFADHI WA MAZAO

Mkulima anapaswa kujua njia zote za kuhifadhi zao lake analolima .Kujua jinsi ya kuhifadhi mazao inamsaidia mkulima kutokupata hasara endapo akikosa soko au soko likiwa halina faida,mkulima ana uwezo wa kuhifadhi zao na kusubiri wakati wa uhitaji wa zao hilo sokoni nahii ndo inafanywa sana na wakulima wa kilimo biashara kwa lengo la kupata faida na kufanikiwa Zaidi kupitia kilimo.Hivyo kabla ya kulima zao ulilokusudia,kwanza jaribu kujua njia za uhifadhi wa zao husika maana uhifadhi wa mazao unatofautiana na kuna njia za asili na njia za kisasa,yote haya mkulima anapaswa kuyatambua lakini piaumakini unahitajika katika uhifadhi wa mazao kwa maana uhifadhi mbaya wa mazao unaweza sababisha uhalibifu wa mazao na kuleta hasara kubwa kwa mkulima.

 

 

 

Imeandaliwa: ADRIA NOLASCO

Mawasialiano: +255 653 827 565

Barua pepe    : adria.nolasco.24@gmail.com

 

 

 

Leave a Reply